728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Monday, May 29, 2017

  UVCCM SIMANJIRO YAMUUNGA MKONO RAIS MAGUFULI

  Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilayani
  Simanjiro Mkoani Manyara, imeungana na wapenda maendeleo nchini
  kumpongeza Rais John Magufuli kwa hatua ya kuzuia usafirishaji mchanga
  wa madini (makinikia) nje ya nchi.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu wa UVCCM wilayani
  Simanjiro, Bakary Mwacha alisema hatua aliyochukua Rais Magufuli ni ya
  kupongezwa na kuungwa mkono na wapenda maendeleo nchini.

  Mwacha alisema kitendo hicho kinapaswa kupongezwa kwani kimeonyesha
  uzalendo na kulinda rasilimali za nchi na kuchukua hatua kwa viongozi
  wazembe waliosababisha hali hiyo.

  Alisema Rais Magufuli alipokuwa anatoa ahadi kwa wananchi kipindi
  anachoomba kura mwaka 2015, kuwa atakuwa mstari wa mbele kulinda
  maslahi ya Taifa ndivyo anavyofanya hivi sasa.“Ni muda mrefu nchi yetu imeibiwa kupitia madini hayo yaliyokuwa yanatoroshwa ila mara baada ya Rais Magufuli kuunda tume na kubaini madudu yaliyopo alikomesha jambo hilo,” alisema.

  Hata hivyo, Mwacha alimpongeza Kaimu Katibu wa UVCCM Taifa, Shaka
  Hamdu Shaka kwa kutoa tamko la kumtetea na kumlinda kwa gharama yoyote
  Rais Magufuli kwa hatua ya kutekeleza mambo ya mabadilikoya kiuchumi
  kisiasa na kijamii. “Sisi jumuiya ya UVCCM wilayani Simanjiro tupo bega kwa bega katika kuhakikisha tunatekeleza na kuunga mkono yale yote yanayotamkwa na
  viongozi wetu wa UVCCM ngazi ya Taifa,” alisema Mwacha.

  Alisema anapongeza jitihada zinazofanywa na Shaka kufanya ziara zake
  za kuzunguka nchi nzima na kuzungumza kwenye vikao vya ndani kwani
  anaimarisha jumuiya hiyo na kuongeza mshikamano wa vijana.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: UVCCM SIMANJIRO YAMUUNGA MKONO RAIS MAGUFULI Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top