728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, May 11, 2017

  UMOJA WA WATANZANIA SWEDEN (TANRIKS) WATOA SALAM ZA RAMBIRAMBI  Sisi watanzania tunaoishi Sweden kwa majonzi na masikitiko makubwa tunatoa pole zetu kuwafikia familia zilizoguswa na msiba, shule ya Lucky Vicent Arusha na Taifa kwa ujumla kwa kupoteza watoto, dereva, na waalimu.  

  Habari hizi zimetugusa sana na kuleta simanzi na masikitiko makubwa katika jamii ya Watanzania hapa Sweden. Tunapendelea pia kuipongeza serikali yetu kwa jitihada zake za kukabiliana na janga hilo bila kupoteza wakati na pia kuwafariji wafiwa katika wakati huu mgumu. 
  TUNATANGULIZA UPENDO NA MSHIKAMANO KWA TAIFA LETU

  KWA NIABA YA WATANZANIA SWEDEN
  MWENYEKITI
  NORMAN JASSON

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: UMOJA WA WATANZANIA SWEDEN (TANRIKS) WATOA SALAM ZA RAMBIRAMBI Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top