728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Wednesday, May 24, 2017

  UBALOZI WA RWANDA NCHINI WAADHIMISHA SIKU YA KUMBUKUMBU YA MAUAJI YA KIMBARI

  Babalozi kutoka nchi mbali mbali wakiwasha mishumaa wakiongozwa na Balozi wa Rwanda nchini Tanzania Mhe. Eugene Kayihura kwenye maaadhimisho ya Kumbukumbu ya Mauaji ya Kimbari dhidi ya Watusi iliyofanyika leo katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Saalam.
   Balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Eugene Kayihura akiongozana na Waziri Mkuu mstaafu, Dkt. Salim Ahmed Salim wakati wakiwasili kwenye Ukumbi wa Mlimani city Jijini Dar es salaam, kulikofanyika Maadhimisho ya  Kumbukumbu ya Mauaji wa Kimbari dhidi ya Watusi yaliyotokea miaka 23 iliyopita huko nchini Rwanda.
  Balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania, Mhe Edzai Chimonyo akizungumza kwenye maadhimisho ya Mauaji ya Kimbari yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
  Balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Eugene Kayihura akizungumza kuhusu mauaji ya Kimbari yaliyotokea nchini Rwanda wakati wa maadhimisho ya miaka 23 yaliyofanyika leo kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
  Waziri Mkuu mstaafu, Dkt. Salim Ahmed Salim  akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 13 ya mauaji ya kimbari ya nchini Rwanda yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
  Nyimbo za mataifa mawili Tanzania na Rwanda zikiimbwa wakati wa maadhimisho ya miaka 23 ya Kimbali nchini Rwanda yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam
  Sheikh Hamis Mtonga akiomba dua wakati wa kuanza maadhimisho ya miaka 23 ya Kimbari ya nchini Rwanda leo.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: UBALOZI WA RWANDA NCHINI WAADHIMISHA SIKU YA KUMBUKUMBU YA MAUAJI YA KIMBARI Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top