728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Wednesday, May 31, 2017

  TIMU YA WILAYA YA UMISETA WILAYANI MBOGWE YAKABIDHIWA BENDERA YA UWAKILISHI MASHINDANO YA UMISETA

   Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri  ya wilaya ya Mbogwe ndg Elias Kayandabila Akiongea na team ya UMISETA ya  Wilaya wakati akifunga mashindano hayo kwa ngazi ya wilaya.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuri  ya Mbogwe Ndg Elias kayandabila akiwakabidhi wanamichezo bendera ya michezo  ya Wilaya 

  Timu ya Wilaya ya UMISETA imekabidhiwa bendera ya michezo ya Wilaya na kutakiwa kwenda kuiwakilisha wilaya kwenye mashindano ya UMISETA
   


  MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBOGWE AFUNGA RASMI MASHINDANO YA UMISETA NGAZI YA WILAYA.

  Timu ya Wilaya ya UMISETA imekabidhiwa bendera ya michezo ya Wilaya na kutakiwa kwenda kuiwakilisha wilaya kwenye mashindano ya UMISETA kwenye ngazi ya Mkoa ambayo yatafanyikia wilayani Geita.

  Akiongea wakati wa kufunga mashindano ya UMISETA ngazi ya Wilaya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe Elias Kayandabila amewataka wanamichezo hao wakacheze kwa bidii na maarifa ili walete ushindi wilayani kwetu

  Pamoja na hayo Mkurugenzi amewataka wakawe na nidhamu ya hali ya juu kwani michezo inahitaji nidhamu na kujituma.

  Kaimu Afisa Elimu Sekondari bi Exvaria Mlowe amemshukuru Mkurugenzi kwa kuiwezesha timu ya wilaya kufanikiwa kwenye maandalizi ya UMISETA ngazi ya Wilaya.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: TIMU YA WILAYA YA UMISETA WILAYANI MBOGWE YAKABIDHIWA BENDERA YA UWAKILISHI MASHINDANO YA UMISETA Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top