728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Monday, May 1, 2017

  RC TABORA AAGIZA VIJANA NA WANAWAKE WAPEWE MIKOPO KUTOKA VYANZO VYA NDANI VYA HALMASHAURI.

  Na Tiganya Vincent, RS-Tabora

  Serikali ya Mkoa wa Tabora imewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote mkoani humo kuhakikisha zinatoa mikopo ya asilimia tano kwa vijana na wanawake ili waweze kujiendeleza katika vikundi vyao na kuwa sehemu ya ajira.

  Agizo hilo limetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri wakati wa kilele cha sherehe za Mei Mosi kwa ngazi ya Mkoa huo.

  Alisema kuwa Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri zote wanapaswa kuhakikisha watoa asilimia hizo kwa wakundi hao mawili kupitia mapato yao ya ndani kama sehemu ya kuyawezesha makundi hayo ili yaweze kutengeneza ajira na kujiingizia kipato na kuondokana na umaskini.

  Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa ajira ya Serikali pekee hazitoshi ni vema wananchi nao wakijiari kupitia kujiunga katika vikundi vikundi na kuanzisha mradi utakaotoa fursa ya ajira kwa watu wengi.

  Aliagiza Wakurugenzi wote Halmashauri kutoa mikopo ya asilimia tano ya mapato yake ya ndani na kisha yeye apate taarifa za orodha na majina ya vikundi na nakala ya kivuli cha hundi ya wanafuika.

  Mkuu Mkoa huyo aliongeza kuwa lengo la serikali ya Awamu ya tano ni kuhakikisha kuwa wananachi wanawezeshwa na kuwekewa mazingira mazuri ya kujiari wenyewe kupitia sekta mbalimbali.

  Alisema kuwa ili kuhakikisha kuwa vikundi vya kimama na vijana wanapata mikopo ya asilimia tano ya fedha zinazotokana na mapato ya Halmashauri ya ndani amewaagiza Mwenyeviti na Meya kusimamia utekelezaji wa agizo lake.

  Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa ametoa wito kwa Halmashauri zote za Mkoa wa Tabora kuweka mazingira mazuri kwa wafanyakazi wapya au wanaohamia ili wavutiwe na kufanyakazi katika mazingira yao.

  Alisema kuwa waige mfano wa Halmashauri nyingine hapa nchini ambazo zimekuwa na utaratibu wa kuwanunulia thamani za ndani na runinga wafanyakazi wapya kama kivutio kwao kupenda kufanyakazi katika maeneo yao mapya.

  Bw. Mwanri alisema kuwa wao wanaweza hata kuwaandalia nafaka kama vile mpunga , maharage na nyumba nzuri ya kuishi ili asiwe kuwaza kuondoa au kuacha kazi kutokana na mazingira magumu.

  Maadhimisho ya Mei Mosi Kimkoa yamefanyika katika Manispaa ya Tabora ambapo kauli mbiu yake ilikuwa ni Uchumi wa Viwanda Uzingatie Haki , Masilahi na Hershima ya Wafanyakazi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: RC TABORA AAGIZA VIJANA NA WANAWAKE WAPEWE MIKOPO KUTOKA VYANZO VYA NDANI VYA HALMASHAURI. Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top