728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Wednesday, May 31, 2017

  MWENGE WA UHURU WAKABIDHIWA WILAYANI UBUNGO UKITOKEA WILAYA YA KINONDONI

  Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mheshimiwa Kisare Makori amekabidhiwa Mwenge wa Uhuru na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Ally Happi tayari kwa kuzuru katika Miradi mitano ya Maendeleo katika Manispaa ya Ubungo.

  Akizungumza wakati wa Makabidhiano hayo Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori amesema kuwa Mwenge wa Uhuru umezuru kwa Mara ya Kwanza katika Wilaya mpya ya Ubungo hivyo historia mpya imeandikwa.

  Alisema kuwa Mwenge wa Uhuru Kwa Mwaka 2017 katika Wilaya ya Ubungo utakimbizwa umbali wa Kilomita 46 na gharama ya Miradi yote Mwenge utakapopita ni Zaidi ya Bilioni 2.8

  Mwenge wa Uhuru Mwenye kauli mbiu ya kutilia msisitizo kushiriki Kukuza Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo ya Nchi yetu umebeba jumbe mbalimbali ikiwemo ile ya Mapambano dhidi ya dawa za kulevya, tuwajali na tuwasikilize watoto na vijana utakapomaliza kutembelea Miradi ya Maendeleo katika Wilaya ya Ubungo utaelekea Mkoani Pwani.

  Katika mbio za Mwenge Umebaba ujumbe mwingine wa kuhamasisha kupungua kwa maambukizi ya Virusi vya Ukimwi, Unyanyapaa na vifo vitokanavyo na UKIMWI.

  Aidha watanzania wameombwa kushiriki kutokomeza Malaria kwa Manufaa ya Watanzia na jamii kwa ujumla.

  Imetolewa Na;
  Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: MWENGE WA UHURU WAKABIDHIWA WILAYANI UBUNGO UKITOKEA WILAYA YA KINONDONI Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top