728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Wednesday, May 17, 2017

  MTAMBO WA KUHAKIKI HUDUMA ZA MAWASILIANO WAPELEKEA SERIKALI KUKUSANYA MABILIONI

  Serikali kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) imekusanya shilingi bilioni 63,015,450,230 kwa kipindi cha Octoba 2013 mpaka Februari 2017 tangu kuanzishwa kwa mtambo wa kuhakiki na kusimamia Huduma za Mawasiliano(TTMS) nchini.
  Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe.Edwin Ngonyani wakati akijibu swali la Mbunge wa Kigamboni.
  “Mtambo huu umesaidia Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) kuongeza ufanisi katika kusimamia Sekta ya Mawasiliano pamoja na kwenda sambamba na kasi ya mabadiliko yanayotokea katika Sekta ya Mawasiliano Duniani kote,”aliongeza Ngonyani
  “Kuanzia Oktoba 2013 hadi Februari 2017, kiasi cha shilingi 63,015,450,230 zilipatika na katika hizo bilioni 56,987,368,631 zimewasilishwa hazina na shilingi bilioni 6,028,081,599 zimewasilishwa Tume ya Sayansi na Teknolojia(COSTECH) kwa ajili ya kugharamia tafiti mbalimbali zenye manufaa kwa nchi yetu ambapo kabla ya mfumo huu mapato hayo hayakuwepo.”
  “Aidha pamoja na mafanikio hayo jitihada za kuboresha zaidi mfumo huu ili kuweza kubaini na kujiridhisha juu ya mapato yote yatokanayo na huduma za mawasiliano na yanayokidhi mahitaji ya Mamlaka ya Mapato Tanzania,Benki kuu ya Tanzania na TCRA zinaendelea,” aliongeza Naibu waziri Ngonyani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: MTAMBO WA KUHAKIKI HUDUMA ZA MAWASILIANO WAPELEKEA SERIKALI KUKUSANYA MABILIONI Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top