728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, May 11, 2017

  Miss tz akabidhiwa gari lake


  Hatimaye Miss Tanzania, Diana Edward Lukumay amekabidhiwa zawadi yake ya gari baada ya kusubiria tokea mwezi Oktoba mwaka jana.

  Kampuni ya Lino International Agency ilishindwa kukabidhi zawadi ya gari kwa wakati baada ya mdhamini wa kwanza aliyeahidi kutoa zawadi hiyo kujitoa hatua za mwisho baada ya shindano hilo kuhamia Mwanza.

  Hatua ya kukabidhiwa zawadi mrembo huyo imetokana na agizo la serikali wa Kampuni ya Lino International Agency kukabidhi zawadi za warembo walioshiriki katika mashindano ya mwaka jana ifikapo mwishoni mwa mwezi huu.

  Kutokana na agizo hilo, kampuni ya Lino International Agency ilianza upya juhudi za kutafuta zawadi kwa mrembo huyo na kuzipata kampuni mbili, kampuni ya uzalishaji na usambazaji wa vipodozi asilia, Grace Product Ltd na duka la kuuza vito ;a Gift Jewellers ambapo kwa pamoja waliamua kununua gari aina ya Suzuki Swift yenye thamani ya Sh milioni 9.

  Mbali ya kununua zawadi hiyo, kampuni hizo pia zililifanikisha usajili wa gari hiyo na kupewa namba ya usajiliwa,T625DKL.

  Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa zawadi hiyo, Diana aiwataka warembo wanaoshiriki katika mashindano ya Miss Tanzania kuwa wavumilivu ili kukabiliana na changamoto mbalimbali za mashindano hayo zinazotokana na matatizo ya kiuchumi.

  “Nimefurahi sana kukabidhiwa gari langu, nimeisubiri kwa muda mrefu na unatakiwa kywa mvumilivu ili kuendelea kuwa na nidhamu, na sasa kwa kupitia gari langu, nitafanya kampeni yangu ya kupiga vita mimba za utotoni na unyanyasaji kwa wanawake kupitia kampuni yake aliyoisajili,” alisema Diana.

  Mrembo huyo pia aliwaomba warembo wajitokeza kushiriki katika mashindano ya hayo pamoja na matatizo yaliyowakumba wao.

  “Mashindano mazuri sana yenye kujenga mtu na kumpatia kipato, tokea nimalize mashindano, nimeweza kupata dili mbalimbali ambazo sikutaka kuziweka wazi kwenye jamii, zimekuwa ni shughuli zangu za kila siku,” alisema.

  Mkuu wa Itifaki wa Kampuni ya Lino, Albert Makoye aliwashukuru wadhamini wao na kwa sasa wanaanza pilika pilika za mashindano ya mwaka huu.

  Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Grace Products ltd, Elizabeth Kilili alisema kuwa ameamua kudhamini zawadi ya gari kutokana na kuvutiwa na mashindano na hasa Diana ambaye anatumia vipodozi vya asili.

  Mhasibu Mkuu wa duka la Gift Jewellers, Faudhia Salum alisema kuwa wamemua kuwezesha zawadi ya gari hiyo, kama moja ya shughuli zao za kijamii. Salum alisema kuwa wao kama wauzaji wa vito wamefarijika sana kusaidia mashindano hayo na hasa ukizingatia kuwa vito vingi uvaliwa na akina dada kwa lengo la kupendeza.
   Ofisa wa Basata akikabidhi funguo kwa Miss Tanzania 2016/2017 Diana Lukumai  kama ishara ya kumkabidhi mrembo  huyo gari yake aina ya Suzuki Swift pembeni yake Mkurugenzi wa Grace Products Ltd Elizabeth Kilili.
   Miss Tanzania 2016/2017 Diana Lukumai akiingia ndani ya gari yake mara baada ya kukabidhiwa
   Miss Tanzania 2016/2017 Diana Lukumai akifurahi mara baada ya kuingia ndani ya gari yake
   Mkuu wa Itifaki wa Kamati ya Miss Tanzania , Arbart Makoye akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi gari
   Mkurugenzi wa Grace Products Ltd Elizabeth Kilili na Mumewe  wakikabidhi kadi ya gari kwa Miss Tanzania 2016/217 Diana Lukumai
   Mkurugenzi wa Grace Products Ltd Elizabeth Kilili. akizungumza na Miss Tanzania 2016/2017 Diana Lukumai katika duka la ke lililopo City Mall jijini Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Miss tz akabidhiwa gari lake Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top