728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Wednesday, May 17, 2017

  MHAGAMA KUFUNGUA MKUTANO WA BODI ZA MIFUKO YA HIFADHI JUU YA UCHUMI WA VIWANDA

  NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA

  WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Walemavu Jenister Mhagama, anatarajiwa kufungua mkutano wa Bodi za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Tanzania.

  Mkutano huo unaoratibiwa na Jumuiya ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Tanzania (TSSA) utafanyika Arusha Mei 19 na 20 mwaka huu,utahusu hatua iliyofikiwa mwaka huu na mada kuu, itakuwa uchumi wa viwana kama fursa ya uwekezaji wa mifuko ya hifadhi ya jamii nchini.

  Pia utaangalia hatua iliyofikiwa ya ushiriki wa mifuko hiyo kwenye uwekezaji wa viwanda na uchumi wa viwanda wenye tija.Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza jana, Katibu Mkuu wa TSSA Meshack Bandawe alisema mkutano huo utakaofunguliwa na Waziri Mhagama, utashirikisha bodi nane za mifuko pamoja na wakuu wa mifuko hiyo ya hifadhi.

  Alisema kwenye mkutano huo Bodi, Wakuu wa mifuko hiyo pamoja na wadau watapata fursa ya kujadili mafanikio , hatua na maendeleo yaliyofikiwa kwenye uwekezaji wa uchumi wa viwanda nchini.

  “ Kwenye mkutano huo tutaangalia mafanikio na hatua iliyofikiwa katika uwekezaji wa viwanda kama fursa muhimu hapa nchini ili uwekezaji wetu uwe na tija ambao utasaidia kukuza uchumi wa nchi na mifuko yenyewe ,”alisema Bandawe.

  Katibu Mkuu huyo wa TSSA alisema kuwa mifuko hiyo imeanza utekelezaji kwwa kuwekeza kwenye miradi mbalimbali ya viwanda na baadhi iko kwenye upembuzi yakinifu.

  Alidai kuwa miradi hiyo ikikamilika itatengeneza ajira kwa vijana wa Tanzania ambao watakuwa wananchama wa mifuko yenyewe na hivyo kuwa na tija katika taifa kwa ujumla.

  Kwa mujibu wa Bandawe nia ya mkutano huo ni kufikia lengo la uwekezaji wa viwanda na utahudhuriwa na Msimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Mamlaka ya Manunuzi ya Umma (PPRA), Benki Kuu (BOT),Wizara ya Viwanda na Biashara, Tume ya Mipango, Msajili wa Hazina na wadau wengine.

  Bandawe alieleza kuwa TSSA inaundwa na mifuko ya hifadhi ya jamii ambayo ni NSSF, PPF,LAPF,PSPF, GEPF,NHIF,WCF na ZSSF.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: MHAGAMA KUFUNGUA MKUTANO WA BODI ZA MIFUKO YA HIFADHI JUU YA UCHUMI WA VIWANDA Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top