728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Sunday, May 7, 2017

  MAKAMU WA RAIS,SAMIA SULUHU HASSAN AWASILI JIJINI ARUSHA JIONI YA LEO

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewasili mjini Arusha jioni hii ambapo hapo kesho ataongoza wananchi wa mkoa wa Arusha na mikoa ya jirani katika kuaga miili ya wanafunzi 32,walimu Wawili pamoja na dereva Mmoja wa shule ya Lucky Visent iliyopo Jijini Arusha waliopata ajali jana tarehe 06-May-2017 katika eneo la Rhotia wilayani Karatu mkoani Arusha.

  Wanafunzi na walimu hao walipata ajali hiyo wakati wanaenda kwenye shule iitwayo Tumaini kwa ajili ya kufanya mitihani wa ujirani mwema baada ya gari walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kutumbukia korongoni kwenye eneo la Rhotia wilayani Karatu.

  Ibada na dua za kuaga miili ya marehemu hao itafanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha kuanzia Saa Mbili asubuhi hapo kesho.

  Katika uwanja wa ndege wa Arusha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan na ujumbe wake wamepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo pamoja na Viongozi wa wengine wa mkoa huo.
   Makamu w a Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo  mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) ambapo  Mhe. Makamu wa Rais ataongoza  wananchi wa mkoa wa Arusha na mikoa jirani kuaga miili ya wanafunzi,na waalimu waliofariki kwenye ajali ya gari. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: MAKAMU WA RAIS,SAMIA SULUHU HASSAN AWASILI JIJINI ARUSHA JIONI YA LEO Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top