728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Monday, May 29, 2017

  MAKALA YA SHERIA: UWEZEKANO WA KUYASHITAKI MAKAMPUNI YA MADINI KUREJESHA HASARA TULIYOIPATA HUU HAPA.  Na  Bashir   Yakub  

  Mikataba yote ya kimataifa huongozwa na wajibu wa aina mbili. Wajibu ulioandikwa(express obligation) na wajibu ambao haukuandikwa(implied obligation). 

  Wajibu ulioandikwa ni masharti yote ya mkataba yaliyo katika maandishi  ambayo wahusika husoma na kuridhia, wakati wajibu usioandikwa ni masharti ya mkataba ambayo hayakuandikwa katika mkataba lakini  yapo kwa asili au yapo kwa kuwa tayari yalishasemwa na sheria na hivyo si lazima kuyaandika katika mkataba. 

  Mathalan, mfanyakazi  wako wa duka hawezi kukuibia halafu akasema kwenye mkataba wangu wa ajira hakuna sharti la uaminifu. Laa hasha  uaminifu  ni sharti la asili "implied obligation" kwa hiyo liandikwe au lisiandikwe  bado lipo tu.Kwenye mikataba ya kimataifa kama ile ya kwetu na makampuni  ya madini masharti yafuatayo ni ya  asili na hayahitaji kuwa yameandikwa ili kuyatekeleza :

  1. Wajibu wa kuanika taarifa zote muhimu kuhusu  shughuli inayotekelezwa katika mkataba( Implied covenant to disclose all necessary information over the subject matter). 
  2. Wajibu wa kutekeleza na kutenda  kwa nia njema(Implied covenant to act in good faith and fair dealing). 

  3. Wajibu wa kila mhusika katika mkataba kuwa  mkweli . Hili huwa ni katazo la udanganyifu(Fraud). 
  Haya yawe yameandikwa kwenye mkataba au hayakuandikwa yakikiukwa tafsiri  yake ni kukiuka masharti ya mkataba.

  Matendo kama kulaghai kuhusu uzito wa madini yanayochukuliwa, kulaghai kuwa unachukua dhahabu huku ukijua unachukua zaidi ya dhahabu, kulaghai kuhusu bei , kutotoa taarifa sahihi za kipi unapata na kipi hupati,nk ni kukiuka wajibu  na masharti ya mkataba jambo ambalo  ni kinyume cha sheria. Na ikiwa wamekiuka mkataba kwa misingi hiyo  basi Tanzania inaweza kufanya yafuatayo. 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: MAKALA YA SHERIA: UWEZEKANO WA KUYASHITAKI MAKAMPUNI YA MADINI KUREJESHA HASARA TULIYOIPATA HUU HAPA. Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top