728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Friday, May 12, 2017

  LG YAZINDUA BIDHAA YA MPYA YA KIYOYOZI INAYOTUMIA UMEME MDOGO NA RAFIKI KWA MAZINGIRA


  KAMPUNI ya vifaa vya Umeme ya Life Good (LG) imezindua viyoyozi ambavyo ni rafiki kwa mazingira kwa gharama za kuweza kumuda kwa kila mtanzania.

  Akizungumza na katika hafla ya uzinduzi wa viyoyozi hivyo , Kaimu Mkurugenzi wa Idara Ushauri wa Wakala wa Majengo Nchini (TBA), Mhandisi Mtapuli Juma amesema vifaa vya LG vina ubora katika matumizi ya nishati ya umeme.

  Amesema kuwa kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi ni muhimu kutumia vifaa vya umeme ambavyo ni rafiki wa mazingira bila kufanya hivyo itakuwa tunaharibu mazingira kwa vizazi vijavyo.

  Amesema kutokana na mabadiliko ya tabia nchi hakuna mtu anayeweza kukwepa katika kutumia vifaa ambavyo vinakuwa ni rafiki wa mazingira.

  Nae Mkurugenzi Mtendaji LG Electronics Afrika Logistics, Janghoon Chung, amesema kuwa wamefanya utafiti na kuona kuna mahitaji ya viyoyozi ambavyo vitakuwa ni rafiki wa mazingira na kutaka watu watumie bidhaa hiyo.

  Amesema viyoyozi hivyo vinatumia nishati ndogo hali ambayo inafanya kila mtu kuweza kumudu matumizi ya viyoyozi pamoja na kulinda mazingira .Aidha amesema kuwa watu wanatakiwa kutumia vifaa ambavyo vinakuwa rafiki wa mazingira ambapo LG wameweza kuzalisha bidhaa kutokana na mahitaji ya sasa yaliyopo.

  Kaimu Mkurugenzi wa Idara Ushauri wa Wakala wa Majengo Nchini (TBA), Mhandisi Mtapuli Juma akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa viyoyozi iliyofanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Legency jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mtendaji LG Electronics Afrika Logistics, Janghoon Chung akingumza na waandishi habari juu ya ubora wa viyoyozi vya LG iliyofanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Legency jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Masoko Afrika Mashariki LG Electronics , Moses Marji akizungumza wakati wa uzinduzi wa bidhaa mpya kutoka LG
  Meneja wa bidhaa za LG Afrika Mhandisi , Singh Chana akizungumza juu ya umuhimu wa bidhaa za LG katika uhifadhi wa Mazingira
  Mkurugenzi Mtendaji LG Electronics Afrika Logistics, Janghoon Chung Akimkabidhi zawadi ya Televisheni mmoja wa washindi wa bahati nasibu iliyochezeshwa katika semina ya uzinduzi wa bidhaa mpya za Lg Tanzania , Ramachandran Veeraman
  Watumbuizaji wa bendi ya Borabora wakiwa wanatoa burudani jukwaani
  Afrika Mashariki Bendi ya muziki ya Borabora ikitoa burudani kwa watu waliofika katika mkutano huo.
  sehemu ya wafanyakazi wa LG wakiwa katika picha ya pamoja
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: LG YAZINDUA BIDHAA YA MPYA YA KIYOYOZI INAYOTUMIA UMEME MDOGO NA RAFIKI KWA MAZINGIRA Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top