728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Friday, May 12, 2017

  KINONDONI YAJIPANGA KATIKA UBORESHAJI WA ELIMU-MANYAMA

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

  Naibu Meya wa Manispaa ya Kinondoni , George Manyama amesema kuwa manispaa imejipanga katika katika kutoa elimu bora kwa wanafunzi.

  Manyama ameyasema hayo katika kilele cha wiki ya elimu kwa Manispaa ya Kinondoni iliyofanyika leo katika shule ya Sekondari ya Mbezi Beach jijini Dar es Salaam amesema watakuwa bega kwa bega na shule zilizo katika manispaa hiyo katika kutoa elimu bora kwa wanafunzi.

  Amesema kuwa katika awamu wa tano wamejipanga katika kutatua changamoto ambazo zinakabili manispaa hiyo ikiwa ni vyumba vya madarasa baada kwa kuisha kwa changamoto ya madawati.

  Mwanafunzi aliyefanya vizuri katika matokeo ya darasa la saba mwaka jana kwa kupata ufaulu wa juu katika shule ya Msingi Mikocheni Islamic , Taus Amiri amesema kuwa alijituma na kuweza kupata ufaulu huo.

  Taus amesema kuwa wanafunzi wenzake wajitume waweze kuwa na ufaulu utaofanya wawe na malengo ya kuendelea kufanya vizuri,Mwalimu Mkuu Msaidizi Mikocheni Islamic, Maulid Omari amesema kuwa shule yao ilikuwa ya pili katika manispaa ya kinondoni kwa kubebwa na Taus kwa kupata alama kubwa katika masomo yote .

  Mama wa Taus , Hiba Msasi amesema mwanae amekuwa na bidii katika masomo ndio maana ilimuwezesha kufanya vizuri katika matokeo ya darasa la saba mwaka jana.
  Naibu Meya wa Manispaa ya Kinondoni , George Manyama akizungumza na waandishi wa habari katika kilele cha maadhimisho ya elimu yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
  Mwanafunzi aliyefanya vizuri katika matokeo ya darasa la saba mwaka jana kwa kupata ufaulu wa juu katika shule ya Msingi Mikocheni Islamic , Taus Amiri akizungumza na waandishi habari juu ya ufaulu wake katika matokeo ya darasa la saba mwaka jana.
  Naibu Meya wa Manispaa ya Kinondoni, George Manyama akitembelea maonesho ya shule katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya elimu .
  Wanafunzi wakifanya maonesho ya kilele cha wiki ya elimu leo jijini Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: KINONDONI YAJIPANGA KATIKA UBORESHAJI WA ELIMU-MANYAMA Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top