728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Friday, May 26, 2017

  DC WA SIMANJIRO AWAASA WANANCHI WA KIJIJI CHA LOSOITO KUITUNZA NA KUTOHUJUMU MIUNDOMBINU YA MAJI

  Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, mhandisi Zephania Ubwani
  akizungumza na wananchi wa kijiji cha Losoito juu ya utunzaji wa
  miundombinu ya maji na maendeleo mengine.

  Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, mhandisi Zephania Chaula
  amewataka wananchi wa Kijiji cha Losoito ,kuitunza na kutohujumu
  miundombinu ya maji yaliyowezeshwa na kampuni ya TanzaniteOne.

  Mhandisi Chaula aliyasema hayo juzi alipofanya ziara ya siku moja
  kwenye kijiji hicho mara baada ya kupatiwa taarifa kuwa kuna baadhi ya
  watu wameharibu miundombinu hiyo kwa kukata mabomba.

  Alisema miundombinu hiyo imewezeshwa kwa pamoja na kampuni ya
  TanzaniteOne na Serikali kwani wanamiliki mgodi huo kwa asilimia 50
  kwa 50 hivyo jamii inapaswa kuyatunza kuyathamini na kuyalinda maji.

  Alisema atamchukulia hatua mtu yeyote atakayekamatwa akiharibu
  miundombinu ya maji kwani wananchi wa eneo hilo kwa muda mrefu
  waliteseka kufuata huduma hiyo umbali mrefu hadi Mirerani.

  “Nimeambiwa awali kuna mama alishajifungua njiani wakati akifuata maji
  na baba wa kimasai akakata kitovu cha mtoto kwa kutumia sime kasha leo
  mtu anaharibu miundombinu hii,” alisema mhandisi Chaula.

  Mkazi wa Kijiji hicho, Magdalena Peter alisema anashukuru kampuni ya
  TanzaniteOne kwa kuwezesha mradi huo wa maji ila bado kuna changamoto
  ya upatikanaji kwani wanayapata mara mbili kwa wiki.

  “Awali tulikuwa tunapata maji hayo kwa wakati fofauti na tulivyokuwa
  tunatembea kilomita 40 hadi Mirerani ila hivi sasa tunawakati mgumu
  baada ya tenki hilo kupasuka,” alisema Peter.

  Ofisa mahusiano wa kampuni ya TanzaniteOne, Halfan Hayeshi alisema
  anaomba apewe muda wa wiki mbili ili ahakikishe anafanyia matengenezo
  sehemu za miundombinu iliyoharibika eneo hilo.

  “Nitakuja na mafundi wiki ijayo ili waangalie na kuikarabati
  miundombinu hiyo na pia tutanunua tenki lenye ujazo wa lita 10,000
  tofauti na hili la lita 5,000 linalotumika hivi sasa,” alisema
  Hayeshi.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: DC WA SIMANJIRO AWAASA WANANCHI WA KIJIJI CHA LOSOITO KUITUNZA NA KUTOHUJUMU MIUNDOMBINU YA MAJI Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top