728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Tuesday, May 30, 2017

  ALEX MSAMA ANG'AKA HABARI ZA KUCHAFULIWA YEYE NA FAMILIA YAKE
  Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mtaa wa Mkwepu Posta jijini Dar es salaam wakati akielezea habari ya gazeti moja la wiki lililoandika habari za kwamba amefilisika na anatafutwa na mahakama,ikiwemo na kudaiwa kuwakimbia Wafanyakazi wake. 

  Akizugumza hayo jijini Dar Es Salaam,Alex Msana amesema yeye ana kampuni nyingi tu,ambazo zote ni zina Wakuregenzi wake na Mameneja wake,ambao wanakwenda kwenye shughuli zao za kiofisi kila siku, na Wafanyakazi wapo na wanaendelea na shughuli zao za kila siku .

  "Sijaona mtu yeyote kutoka Mahakamani akileta ujumbe wa yeye kuitwa mahakamani, lakini pia hakuna hata taarifa ya yeye kuitwa polisi kwa tuhuma yoyote kama ilivyodaiwa kwenye hilo gazeti,hivyo habari hizo ni za uzushi na zinalenga kumpaka matope, lakini baya zaidi zinaihusisha familia yake" alisema Msama . 

  Msama amesema kuwa ni kweli amepungunza Wafanyakazi,hasa katika kitengo cha uchapishaji wa Magazeti,ili kukidhi hali halisi ya sasa,na kwamba kampuni yake si ya Kwanza kupunguza Wafanyakazi,anasema kufuatia hatua hiyo amekuwa akisikia maneno na mengine yakisambazwa kwenye mitandao ya kijamii yenye lengo la kumchafua yeye pamoja na familia yake.

  Amesema kwa sasa ameamua kuchukua hatau,anajadiliana na wanasheria wake ili kuchukua hatua za kisheria kuwafikisha mahakamani wahusika, kwa sababu wamelenga kumvunjia heshima yeye, kampuni zake na familia yake mbele ya jamii ya Watanzania. 

  Amesema kuwa mara baada ya kuandaa utaratibu wa kisheria, watapeleka mashtaka mahakamani ili kudai haki yake ya msingi ya udhalilishaji uliofanywa na wahusika hao. 
   
  Msama amewaasa Waandishi wa Habari kutumia kalamu zao vizuri sambamba na weredi wao katika majukumu makubwa ya kuielemisha jamii,katika masuala muhimu,ikiwemo na kujenga Nchi kwa kila nyanja husika,na si kukaa na kutunga ama kuzusha habari zisizokuwa na ukweli wowote.

  Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari jana  kuhusiana na Madai yake kuchafuliwa yeye na Familia yake kupitia gazeti moja litakalo kwa wiki.
  Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akionesha kukerwa na habari hizo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye moja ya ofisi zake jijini Dar es salaam jana
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: ALEX MSAMA ANG'AKA HABARI ZA KUCHAFULIWA YEYE NA FAMILIA YAKE Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top