728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Sunday, April 23, 2017

  WAZIRI MHAGAMA: MAANDALIZI YA SHEREHE ZA MIAKA 53 YA MUUNGANO YAKAMILIKA

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Jenista Mhagama ameeleza kukamilika kwa maandalizi ya kuadhimisha sherehe za miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zitakazofanyika Viwanja vya Jamhuri Mjini Dodoma, siku ya jumatano Aprili 26, 2017.

  Ameyasema hayo leo wakati akizungumza waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika Aprili 22, 2017 katika Ofisi yake Dodoma.

  “Nipende kuwaeleza Watanzania wote kuwa hadi sasa maandalizi ya kuifikia siku ya Maadhimisho ya Sherehe za Muungano tayari yamekamilika kwa kuangalia mambo yote yaliyopangwa katika ratiba ambapo mgeni rasmi atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli.”Alisema Waziri Mhagama.

  Amesema sherehe hizo zitakuwa na  upekee wa aina yake ukizingatia kuwa  ni mara ya kwanza tangu Serikali ilipotimiza adhma yake ya kuhamia Dodoma.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi, Ajira na watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Dodoma kuhusu Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yatakayofanyika Mkoani Dodoma 26 Aprili 2017.Kulia kwake ni  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.Januari Makamba na kushoto  ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Jordan Rugimbana.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.Januari Makamba akizungumza na waandishi wa habari leo Mjini Dodoma kuhusu matukio mbalimbali yatakayokuwepo katika Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yatakayofanyika Mkoani Dodoma 26 Aprili 2017.Kushoto kwake ni  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi, Ajira na watu wenye Ulemavu Mhe,Jenista Mhagama na mwishoni ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bw.Jordan Rugimbana.
  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Jordan Rugimbana akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) juu ya maandalizi ya Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yatakayofanyika Mkoani Dodoma 26 Aprili 2017 na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi.Kulia kwake ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi, Ajira na watu wenye Ulemavu Mhe,Jenista Mhagama na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.Januari Makamba.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: WAZIRI MHAGAMA: MAANDALIZI YA SHEREHE ZA MIAKA 53 YA MUUNGANO YAKAMILIKA Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top