728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, April 6, 2017

  WAZIRI MAHIGA AZUNGUMZA NA MKURUGENZI WA UN WOMEN KWA KANDA YA MASHARIKI NA KUSINI MWA AFRIKA

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake cha Umoja wa Mataifa (UN Women) kwa Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bi. Izeduwa Derex-Briggs alipofika Wizarani tarehe 06 Aprili, 2017. Katika mazungumzo yao, Bi. Derex-Briggs alimweleza Mhe. Waziri maendeleo ya utendaji wa Kitengo hicho kwa Kanda na umuhimu wa uwepo wao hapa nchini. Pia alimtambulisha Bi. Hodan Addou, Afisa Msimamizi mpya  wa Kitengo hicho hapa nchini. 
  Mhe. Mahiga akiendelea na mazungumzo na Bi. Derex-Briggs huku Bi. Hodan Addou (kushoto), Afisa Msimamizi mpya wa Kitengo cha Wanawake cha Umoja wa Mataifa hapa nchini na Bi. Sekela Mwambegele (kulia), Afisa Mambo ya Nje wakifuatilia. 
  Bi. Derex-Briggs nae akimweleza jambo Mhe. Waziri 
  Hapa Bi. Derex-Briggs (katikati) akimtambulisha rasmi Bi. Addou kwa Mhe. Mahiga 
  Picha ya pamoja
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: WAZIRI MAHIGA AZUNGUMZA NA MKURUGENZI WA UN WOMEN KWA KANDA YA MASHARIKI NA KUSINI MWA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top