728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Sunday, April 30, 2017

  WAWILI WAONDOKA NA PIKIPIKI SHIKA NDINGA BAGAMOYO

   Meneja wa Matukio na Mawasiliano wa Efm Radio, Neema Ukurasi Akizungumza na wakazi wa Wilaya ya Bagamoyo juu Shindano la Shika Ndinga ambalo limeweza kuwazawadia washindi wawili pikipiki aina ya Sunmoto  mara baada ya kufanikiwa kupita katika vipengele vyote katika shindano lililofanyika shule ya Msingi Majengo Bagamoyo
   Meneja wa Matukio na Mawasiliano wa Efm Radio, Neema Ukurasi akikabidhi  Pikipiki kwa mshindi kwa upande wa kina Dada Kawale Halidy  ambaye ameweza kuondoka na pikipiki ya SUNMOTO
   Meneja wa Matukio na Mawasiliano wa Efm Radio, Neema Ukurasi akikabidhi zawadi ya pikipiki kwa Mshindi wa Shika Ndinga upande wa Wanaume , Valerian Gilbert katika shindano lililofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Majengo Bagamoyo.
   Said Magongo akimbusu mkewe Kawale Halidy mara baada ya kufanikiwa kuondoka na pikipiki ya Sunmoto katika shindano la shika ndinga lililofanyika mkoa wa Pwani Wilaya ya Bagamoyo.
   Washiriki upande wa kina Dada wakiwa katika zoezi la mbio za kukimbia na vikombe vya maji
   Mchekeshaji kutoka Efm akitoa burudani kwa wakazi wa Wilaya ya Bagamoyo
   Washiriki wa shika ndinga upande wa Wanaume wakiwa katika hatua ya kujaza vikombe na kukimbia navyo
   Msanii wa michezo ya Sarakasi za Baiskeli , Junior Talent akiwa amekaa juu ya Baiskeli kwa satili isiyokuwa ya kawaida na kuwashangaza wakazi wengi wa Bagamoyo

   Majaji wakimshusha mmoja wa washiriki katika kipengele cha mwisho cha Shindano la Shika Ndinga
   Washiriki upande wa kiume wakiwa wameshikilia gari kisawa sawa katika hatua ya mwisho ya shindano hilo
  Mmoja wa Watangazaiwa EFM radio akizungumza na wakazi wa bagamoyo walifurika katika kiwanja cha Shuleya msingi Majengo
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: WAWILI WAONDOKA NA PIKIPIKI SHIKA NDINGA BAGAMOYO Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top