728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Tuesday, April 25, 2017

  WATUHUMIWA WA UGAIDI BAADHI WAGOMA KUSHUKA KATIKA GARI LA MAGEREZA

  Na Pamela Mollel,Arusha

  Katika hali isiyokuwa ya kawaida Mahabusu wanaotuhumiwa na ugaidi jijini Arusha baadhi yao leo wamegomea kushuka katika gari la magereza kwa madai kuwa hawatendewi haki kwa kesi zao kutosikilizwa hali inayowalazimu kukaa mahabusu kwa muda mrefu bila kujua hatima yao

  Tukio hilo lilitokea katika viwanja vya mahakama majira ya saa 9:27 asubuhi ambapo tukio hilo lilisimamisha shughuli za mahakama kwa muda wa zaidi ya masaa mawili huku baadhi ya watuhumiwa wengine wa ugaidi wakivua nguo zao kushinikiza kesi zao kusomwa

  Mahabusu 32 tu ndio waliokubali kushuka katika gari hilo na kuingia mahakamani huku 29 wakigomea kushuka na kubakia ndani ya gari hali iliyozua taharuki kwa baadhi wa watu walikuja kufatilia kesi hiyo

  Hakimu mkazi wa mahakama hiyo Nestory Baro aliwataka watuhumiwa hao kuwa wavumilivu, kwa kuwa kesi yao ipo katika hatua za mwisho huku akiwasii kutogomea kuja mahakamini kwa kufanya hivyo wanajinyima haki yao ya kisheria

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti mahakamani hapo watuhumiwa hao Shabani Idi na Yusuph Alli waliiomba mahakama kuharakisha kesi hiyo kwa kuwa familia zao zinaishi katika wakati mgumu 

  “Mtoto wangu wa darasa la nne amekatisha masomo anaokota makopo kwaajili ya kuuza ili familia wapate chakula pamoja na wadogo zake kupata nauli ya shule”alisema Shabani 

  Aidha waliongeza kuwa familia zao sasa zipo hatarini kuingia katika makundi mabaya ya tabia kutokana na wazazi wao kuwa mbali nao hivyo wao kuendelea kuwepo magerezani ni changamoto kubwa sana kwa familia zao
  Mahabusu wanaotuhumiwa na ugaidi jijini Arusha leo baadhi yao wamegomea kushuka katika gari la magereza kwa madai kuwa hawatendewi haki kwa kesi zao kutosikilizwa hali inayowalazimu kukaa mahabusu kwa muda mrefu bila kujua hatima yao.
  Watuhumiwa wa ugaidi baadhi yao wakiingia katika gari la magereza baada ya 32 kutii amri ya mahakama
  Watuhumiwa wa ugaidi wakiwa katika viwanja vya mahakama leo jijini Arusha
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: WATUHUMIWA WA UGAIDI BAADHI WAGOMA KUSHUKA KATIKA GARI LA MAGEREZA Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top