728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Saturday, April 22, 2017

  SHINDA NYUMBA AWAMU YA PILI: DROO NDOGO YA TATU KUFANYIKA VIWANJA VYA BAKHRESA, MANZESE

  ILE droo ndogo ya tatu ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili, iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu, sasa itafanyika katika Viwanja vya Bakhresa, vilivyopo Manzese jijini Dar es Salaam, Aprili 26, mwaka huu. Afisa Masoko wa Global Publishers, ambayo ndiyo waendeshaji wa bahati nasibu hiyo, Yohana Mkanda alisema jijini jana kuwa, droo hiyo itachezeshwa katika viwanja hivyo kuanzia saa nane mchana hadi 12 jioni.
  Wasomaji wa Magazeti ya Global Publishers, wakichangamkia Gazeti la Ijumaa na Championi kabla ya Droo ya Pili ya Shinda Nyumba kuanza.
  “Mipango yote kwa ajili ya shughuli hiyo imekamilika, tunawaomba wasomaji wetu kuendelea kuhifadhi kuponi zao na kujitokeza kwa wingi siku hiyo, kwani kama tulivyoahidi, zawadi kibao zitatolewa na washindi watatangazwa mubashara,” alisema Mkanda. Zawadi zitakazotolewa katika droo hiyo ya tatu ni pamoja na pikipiki, seti ya televisheni flat screen, simu ya kisasa za mkononi pamoja na dinner set ambapo washindi watapatikana hapohapo Manzese kwa Bakhresa. Droo hiyo ndogo ya tatu itafanyika baada ya mbili za awali, ambazo washindi walipata zawadi kama hizo kufanyika katika maeneo ya Mbagala ndani ya Ukumbi wa Dar Live na Mwananyamala katika Viwanja vya CCM Mwinjuma. Global Publishers, wachapishaji wa magazeti ya Ijumaa, Uwazi, Risasi, Championi, Amani na Ijumaa Wikienda ni kampuni pekee ya uchapaji magazeti kuwahi kutoa zawadi kubwa ya nyumba nchini katika bahati nasibu. Ili kupata kuponi hizo, msomaji anatakiwa kununua mojawapo ya magazeti ya kampuni hiyo na kujaza kuponi zilizopo ukurasa wa pili wa magazeti hayo na kuzipeleka kwa mawakala waliopo nchi nzima na kwa wale wa Dar, wanaweza kupeleka ofisi za Global zilizopo Bamaga, Mwenge.
  Kuponi zikichanganywa.
  Bahati nasibu hiyo ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili imedhaminiwa na British School waliopo karibu na Kituo cha Daladala cha ITV na Kanisa la Lutheran Mwenge na Kilimanjaro Institute of Technology waliopo Mwenge kwa MamaNgoma na Sinza Mori.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: SHINDA NYUMBA AWAMU YA PILI: DROO NDOGO YA TATU KUFANYIKA VIWANJA VYA BAKHRESA, MANZESE Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top