728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Tuesday, April 4, 2017

  SERIKALI YAWASAHURI WANANCHI KUTOKUWA TEGEMEZI.

  Na Raymond Mushumbusi WHUSM Dodoma

  Serikali imewasahuri wananchi wote wanaofaidika na Mpango wa kunusuru Kaya Maskini (TASAF) nchini kuzitumia vizuri ruzuku wanazozipata kwa kuendelea kujishughulisha na shughuli za kiuchumi katika maeneo yao.

  Akijibu swali la Mbunge wa Mtabwe Mhe. Khalifa Mohamed Issa lililouliza Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) upo katika Awamu ya Tatu ya Utekelezaji wa Mpango wa kunusuru Kaya Maskini nini kimefanyika ili ruzuku ziweze kumudu mahitaji ya chakula, Elimu, Afya na lishe Bora kwa watoto.

  Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki amesema kuwa Serikali inaendelea kutoa ruzuku wa Kaya Maskini ila inasahuri pia wananchi waendelee kujishughulisha na kazi nyingine za kuongeza kipato na isitegemee ruzuku pekee.

  “Niwaombe wananchi wanaopata ruzuku kutoka mpango wa TASAF wajishughulishe pia na shughuli nyingine za kiuchumi na kutotegemea ruzuku pekee” Alisistiza Mhe. Angella.

  Ameongeza kuwa ruzuku zinazotolewa ni kichocheo cha kuifanya kaya iweze kujikimu hasa katika kupata mahitaji muhimu huku ikiendelea kujiimarisha kiuchumi kwa kuweka akiba na kutekeleza miradi ya ujasiriamali ili iweze kusimama yenyewe na kujitegemea baada ya kutoka katika umaskini uliokithiri.

  Mhe. Angella Kairuki ameeleza kuwa vigezo vya kupata kaya maskini ni wa uwazi na huanishwa na Jamii katika mkutano wa hadhara unaoendeshwa na wawezeshaji kutoka Halmashauri za Wilaya na kusimamiwa na Viongozi wa Vijiji, Mitaa na Shehia.

  Aidha uzoefu uliopatikana umeonesha kwamba kwa kiwango cha ruzuku kinachotolewa kwa wananchi wanaofaidika na Mpango huo kimewawezesha kuboresha maisha yao kwa kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi zikiwemo ufugaji,ujasiriamali na  ujenzi wa nyumba bora, hivyo viwango hivyo sio vidogo kama wengi wanavyodhani.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha kwanza cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 Mjini Dodoma.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: SERIKALI YAWASAHURI WANANCHI KUTOKUWA TEGEMEZI. Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top