728x90 AdSpace

 • Habari za hivi Punde

  Monday, April 3, 2017

  PELEKENI WATUMISHI WAKAPIGWE MASASA TPSC- WAZIRI KAIRUKI

  Serikali imewaagiza waajiri wote na watumishi wa umma kwa ujumla wao, kukitumia chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kwa mafunzo mbalimbali yanayolenga kuboresha fani na taaluma zilizopo katika sehemu za kazi. 

  Akizungumza mwishoni mwa wiki katika mahafali ya 26 ya TPSC Mkoani Tabora, Waziri wa nchi Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora) Angellah Kairuki, akisema Chuo hicho kikitumiwa ipasavyo, ufanisi sehemu za kazi utaongezeka. 

  “Kwa nafasi yangu kama waziri mwenye dhamana ya utumishi wa umma na kwa kushirikiana na viongozi wenzangu, tunaahidi kukijengea chuo uwezo na kukiongezea ufanisi katika utoaji huduma ya taaluma bora na ujuzi katika maeneo yetu ya kazi,”alisema. 

  Alisema serikali siku zote imejitahidi kuhakikisha kwamba TPSC inatoa kozi ambazo zinatambulika katika mfumo wa elimu ili wahitimu waweze kukubalika katika soko la ajira badala serikali peke yake. 
  Waziri wa nchi Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora) Angellah Kairuki akizungumza wakati ma mahafali ya 26 ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania(TPSC) mjini Tabora hivi karibuni.
  Meza kuu, akiwamo Mtendaji Mkuu wa TPSC Dk.Henry Mambo (Wa tatu kushoto) akifuatilia hotuba ya Waziri wa nchi Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora) Angellah Kairuki wakati wa mahafali ya 26 ya TPSC yaliyofanyika TPSC tawi la Tabora mwishoni mwa wiki.
  Mkurugenzi wa Chuo Cha Utumishi wa Umma, Tawi la Tabora, Hussein Simon Lufunyo, akimweleza jambo Waziri wa nchi Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora) Angellah Kairuki wakati Waziri huyo alipotembelea jingo la chuo hicho linalojengwa kwa ajili ya madarasa na ofisi,wa pili kushoto Dk.Charles Msonde Mwenyekiti wa Bodi ya Taaluma ya chuo hicho, Wa nne kushoto ni Mtendaji Mkuu wa TPSC Dk.Henry Mambo
  Mtendaji Muu wa TPSC Dk.Henry Mambo akifuatilia kwa makini moja ya matukio wakati wa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora) Angellah Kairuki, alipotembelea jengo la ghorofa tawini hapo, jengo hilo litatumika kwa madarasa na ofisi 
  Serikali imewaagiza waajiri wote na watumishi wa umma kwa ujumla wao, kukitumia chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kwa mafunzo mbalimbali yanayolenga kuboresha fani na taaluma zilizopo katika sehemu za kazi.

  Akizungumza mwishoni mwa wiki katika mahafali ya 26 ya TPSC Mkoani Tabora, Waziri wa nchi Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora) Angellah Kairuki, akisema Chuo hicho kikitumiwa ipasavyo, ufanisi sehemu za kazi utaongezeka.

  “Kwa nafasi yangu kama waziri mwenye dhamana ya utumishi wa umma na kwa kushirikiana na viongozi wenzangu, tunaahidi kukijengea chuo uwezo na kukiongezea ufanisi katika utoaji huduma ya taaluma bora na ujuzi katika maeneo yetu ya kazi,”alisema.

  Alisema serikali siku zote imejitahidi kuhakikisha kwamba TPSC inatoa kozi ambazo zinatambulika katika mfumo wa elimu ili wahitimu waweze kukubalika katika soko la ajira badala serikali peke yake.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: PELEKENI WATUMISHI WAKAPIGWE MASASA TPSC- WAZIRI KAIRUKI Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top