728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Monday, April 3, 2017

  NAIBU WAZIRI MAVUNDE KUNOGESHA TAMASHA LA PASAKA MKOANI DODOMA


  Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu maandalizi ya tamasha hilo litakalofanyika Aprili 16,2017 kwenye Uwanja wa Uhuru.

   
  Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama amesema kuwa wakati uzinduzi wa tamasha la pasaka April 16,2017 katika Uwanja wa Uhuru, mgeni rasmi akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Mchemba atakayemwakilisha Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, mgeni rasmi katika Uwanja wa Jamhuri, mkoani Dodoma atakuwa ni Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavumde.

  Msama alisema baada ya Tamasha hilo kutikisa vilivyo katika Uwanja wa Jamhuri mbele ya Naibu Waziri Mavunde ambaye pia ni Mbunge wa Dodoma mjini, tamasha hilo litahamia katika jiji la Mwanza, Simiyu na Iringa.

  Alisema kamati yake imeamua kuufikia mji wa Dodoma kutokana na watu wake kulipenda Tamasha hilo, pia heshima ya Dodoma kama mji mkuu wa nchi na makao makuu ya serikali.

  "Pamoja na mambo mengine yanayokwenda na tukio hilo, malengo ya msingi ni kueneza ujumbe wa Neno la Mungu, pia kutumia sehemu ya mapato kufariji watoto yatima, walemavu na wajane".alisema Msama

  Wakati huo huo,Msama alisema kuwa katika tamasha hilo Albamu mpya ya ‘Jitenge na Ruth’ ya malkia wa muziki wa injili kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, Rose Muhando, itazinduliwa rasmi.

  Msama amesema kuwa,Rose Muhando mwimbaji nguli wa nyimbo za injili nchini ambaye amekuwa akishiriki mara kwa mara katika tamasha hilo,kwa mara nyingine atalitumia jukwaa hilo la tamasha la Pasaka kuzindua albamu yake.

  Akizungumza jijini Dar es Salaam ,Alex Msama ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo,alisema albamu hiyo yenye nyimbo kibao, itazinduliwa April 16 katika Uwanja wa Uhuru.

  Msama alisema tukio la uzinduzi wa albamu hiyo na ile ya ‘Ngome Zimeanguka’ ya Kinondoni Revival, anaamini Tamasha la mwaka huu litakuwa tofauti.

  Alisema uwepo wa Rose, Kinondoni Revial Choir, Kwa ‘Viumbe Vyote’ ya Tabora na Solly Mahlangu kutoka Afrika Kusini na wengine mahiri, ni faraja kubwa kwa wadau wa Tamasha hilo.

  Msama alisema, baada ya uzinduzi wa nguvu katika Uwanja wa Uhuru, siku itakayofuata uhondo huo utahamia Uwanja wa Jamhuri, mjini Dodoma.


  Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama, akifafanua kwa kina uzinduzi wa albamu mbili,katika tamasha la pasaka  litakalofanyika Aprili 16 kwenye Uwanja wa Uhuru.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: NAIBU WAZIRI MAVUNDE KUNOGESHA TAMASHA LA PASAKA MKOANI DODOMA Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top