728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Wednesday, April 12, 2017

  MIRADI VIPORO KUKAMILIKA KABLA YA MWEZI JUNI, 2017


   Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Athumani Kihamia akiwakumbusha watumishi wa kwenye Kata (hawapo Pichani) kutekeleza yale yote yaliyoainishwa kwenye Ila ni ya Chama cha Mapinduzi katika utendaji kazi wao wa Kila siku.
  A 2
  Baadhi ya Watumishi wa Kwenye Kata za Muriet naTerrati wa kifuatilia Kikao
  A 3
  Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Athumani Kihamia(Kulia) akiwa na Afisa Tawala wa Jiji Ndg. Frank Sanga kwenye Kikao na Watendaji wa Kata
  A 4
  Mtendaji wa Kata ya Muriet Joachim Kisarika (Pilikushoto) akitoa taarifa kwa Mkurugenzi wa Jiji na Ujumbe wake kuhusu Ujenzi wa Kituo cha Polisi Kata yaMuriet.
  A 5
  Ujenzi wa Kituo cha Polisi Muriet umefika hatua ya mtamba wa panya, Kituo hiki kinajengwa na mdau wa maendeleo.
  …………..
  Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Ndg. Athumani Juma Kihamia amewaagiza watendaji wa Kata kukamilisha miradi yote viporo iliyopo kwenye  Kata kabla ya kuanza kutekeleza miradi mipya iliyopitishwa katika kata husika.
  Kihamia ameyasema hayo wakati akizungumza na watumishi wa Serikali katika Kata ya Muriet na Terati wakati wa ziara ya keyakutembelea Kata zote 25 zaJiji la Arusha na ambapo ziara hiyo imekamilika katika kata ya Muriet.

  Amesema kuwa lengo hasa la kutembelea Kata zote na kuonana na watumishi hao ni kuwakumbusha watumishi wajibu wao na kufanya kazi kwa kuzingatia Miiko na Maadili ya Serikali huku na kuhakikisha kwamba shughuli zote za kwenye Kata zinafanyika kwa kuzingatia Sheria, kanun, taratibu na miongozo iliyopo. 

   “Siyo kwamba watumishi wangu wa Halmashauri hawafanyi kazi bali ni kuwakumbusha majukumu yao katika kutumikia wananchi hasa katika kasi ya Serikali ya awamu ya tano ya hapa kazi tu ambayo inatutaka tuwekaribu zaidi na wananchi wetu na Mimi kama Mtendaji Mkuu lazima nisimamie kikamilifu“Alisema Mkurugenzi Kihamia.

  Kupitia  Kikao  hicho amewataka watendaji wote Kuhakikisha kwamba Miradi viporo iliyopo kwenye Kata na Mitaa inakamilika kabla ya mwezi Juni ili kuweza kuleta Tija kwa wananchi na sikuanza kutekeleza miradi mipya nakuacha Fedha na nguvu zikipotea katika miradi ya miaka ya nyuma ambayo haikukamilika.

  Alisema kuna miradi ya mwaka 2015/2016 ambayo Fedha zimeshakutumika lakini haikukamilika sasa endapo tutaiacha tena mwaka huu miradi hiyo itaanza kuharibika na kukosa thamani kabisa hivyo tukapoteza Fedha za Serikali ambazo zilishaingizwa kwenye miradi hiyo ni vyema tukaikamilisha ndipo tuanze miradi mipya.

  Vile vile alisema kuwa watendaji wa Serikali wanatakiwa wajitume kwa nguvu zote wasisubiri mpaka  viongozi wa juu wafike kwenye maeneo yao na wananchi walalamike wakati kuna kiongozi katika maeneo hayo ambao wanalipwa na Serikali ilikusaidia wananchi.

   ” Hatutaki Mwananchi atoke kwenye Kata mpaka kwa Mkuu wa Mkoa au Mkuu wa Wilaya kwenda kulalamikia masuala madogo  madogo wakati kuna kiongozi ambaye tumemuweka ili atatue kero akitokea Mtumishi wa hivyo ajue kwamba hatoshi kuongoza wananchi” Alisema Kihamia.
  Ameongeza kuwa kwasasa anahakikisha Huduma zinaboreshwa katika Jiji la Arusha kwa kumjengea Mtumishi uwezo wa kufanya kazi bila kuogopa changamoto zilizopo na kuwajasili wakati anaongoza wananchi kwenye maeneo yao.

  Hata hivyo amewagiza watumishi hao wa Serikali wakiwemo watendaji kutekeleza kwa muda uliowekwa mambo muhimu kama Utoaji wa Mikopo kwa vikundi vya vijana na Wanawake, kuainisha biashara zilizopo kwenye maeneo yao ya Utawala ikiwemo idadi ya mabango na maduka yote, majengo na maeneo ya wazi pamoja na miradi viporo
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: MIRADI VIPORO KUKAMILIKA KABLA YA MWEZI JUNI, 2017 Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top