728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Monday, April 3, 2017

  MGOMO WA MABASI YA MIKOANI NA DALADALA WASITISHWA RASMI


  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii 
   
  Mamlaka ya udhibiti wa Usafiri na Nchi Kavu (Sumatra) pamoja na wadau wa sekta ya usafirishaji wamekubaliana kusitisha mgomo wa usafirishaji wa abiria na mizigo uliotakiwa kuanza kesho.
   
  Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Sumatra, Gilliard Ngewe amesema kusitisha huko kunatokana na kikao na waziri mwenye dhamana, Profesa Makame Mbarawa juu ya kuandika kwa kutenganisha makosa ya dereva na wamiliki.
   
  Amesema kanuni hizo zitaandikwa ndani ya siku 14 katika rasimu hiyo na wadau wa usafirishaji kuendelea usafirishaji.
   
  Ngewe amesema kuwa baada ya kufanya marekebisho ya rasimu ya kanuni itarudishwa kwa wadau kuweza kujadiliwa kwa ajili ya kupeleka bungeni.
  Nae Makamu Mwenyekiti wa Wamiliki wa Mabasi, Abdallah Mohamed amesema wamekubaliana na Sumatra mambo ambayo hayakuwa sawa warekebishe katika kanuni za makosa kati ya wamiliki na madereva wa mabasi.
   
  Amesema wasipokubaliana baada ya siku 14 watarudi katika mkutano mwingine kwa kila mmoja namna gani ya kuweza kutengeneza sheria ambazo haziathiri upande mmoja.Mwenyekiti wa wamiliki wa Daladala , Kasmat Jaffer amesema suala ambalo limekuwa mwiba ni kosa la kufungwa pamoja na faini hali ambayo wameona ni bora kuachana na biashara hiyo.
   
  Picha ya Maktaba Yetu,
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: MGOMO WA MABASI YA MIKOANI NA DALADALA WASITISHWA RASMI Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top