728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Tuesday, April 25, 2017

  kova atunukiwa tuzo ya heshima na apec


  Shirika lisilo la kiserikali la APEC, Respicius Timanywa limempatia tuzo ya heshima, aliyekuwa Kamanda wa Polisi Kanda maalumu ya Dares Salaam, Suleiman wakati wa uzinduzi wachuo hicho kwa kuwezesha madereva bodaboda zaidi ya 350,000 kupata mafunzo ya aina mbali mbali chuoni hapo.

  Kabla ya kutolewa kwa tuzo hizo, Timanya alitoa wito na kuhamasisha wananchi hasa madereva bodaboda kulaani mauji ya polisi na kujenga utamaduni wa kuwakinga na majanga kwa kuhakikisha wanatoa taarifa kwa wakati.
  Amesema tukio la mauji ya polisi  lililotokea Aprili 13,mwaka huu,Mkengeni Kata ya Njawa wilaya ya Kibiti mkoani Pwani lilifanywa na wahalifu ambapo linadhihirisha yalidumu kwenye maeneo hayo kwa muda mrefu.

  Amesema, anaimani mafunzo hayo ya bodaboda itawawezesha kutambua kuwa ulinzi na usalama ni wajibu wa kila mtanzania hivyo  kila mtu mwenye taarifa, tukio ama mtu anayemtilia shaka apeleke taarifa polisi.
  Amewaomba waendesha bodaboda 350,000 waliopatiwa mafunzo ya usalama barabarani na Shirika hilo nchini kuzindua kampeni ya kulaani mauji ya polisi na kuhamasisha wananchi kuwa ni wajibu wao kuwakinga.

   Kamishna wa kazi Hilda Kabisa akiangalia sola ya kuchemshia maji wakati wa uzinduzi wa chuo cha Apec jijini Hapa.
  Kova akionesha cheti cha heshima alichopewa na chuo hicho.
  Kova na Mkurugenzi wa chuo cha Apec wakiwa katika picha ya pamoja
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: kova atunukiwa tuzo ya heshima na apec Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top