728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Saturday, April 15, 2017

  DUKA LA KISASA LA GSM MALL LAUNGUA MOTO DAR

   Magari ya Zimamoto na Uokoaji yakiwa nje ya Duka kubwa la GSM Mall tayari kuzima moto uliokuwa unaunguza duka hilo katika Barabara ya Nyerere eneo la Mtava, Dar es Salaam. Chanzo cha moto huo hakikuweza kujulikana mara moja. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
   Mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo akiwahishwa hospitali.
   Pilikapilika katika lango kuu la kuingilia duka hilo

   Mmoja wa majeruhi akitolewa kwenda kwenye gari ili awahishwe hospitali kwa matibabu
  Wananchi wakishuhudia ajali hiyo ya moto


  Na Richard Mwaikenda 

  DUKA kubwa la GSM Mall ililopo Barabara ya Nyerere eneo la Mtava, Dar es Salaam, linateketea kwa moto hivi sasa.

  Kwa mujibu wa mashuhuda ni kwamba duka hilo lilianza kuungua majira ya 8;30,Hadi sasa chanzo cha moto huo hakijaweza julikana. 

  Magari ya zimamoto na uokoaji yamejazana eneo hilo kunusuru mali na maisha ya watu waliokuwemo kwenye jengo hilo lenye ghorofa nne.

  Watu wengi wakiwemo wafanyakazi wa duka hilo walionekana kutoka mkuku kuokoa maisha yao. Baadhi yao walitolewa wakiwa mahututi na kukimbizwa hospitali kwa kutumia magari ya polisi.

  Duka hilo kubwa la kisasa lenye maduka yenye aina mbalimbali za bidhaa ni moja kati ya maduka makubwa yaliyopo jijini Dar es Salaam.

  Waokoaji waliokuwepo wamepata wakati mgumu kuzima moto kutokana na ndani ya jengo hilo kuwa na giza nene lililotawaliwa na wingu la moshi uliosababishwa na moto huo.

  Wamejitahidi kupata mwanga kwa kuwasha taa za magari karibu na lango kuu la kuingilia ndani lakini ilishindikana.

  Mwisho
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: DUKA LA KISASA LA GSM MALL LAUNGUA MOTO DAR Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top