728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Friday, April 21, 2017

  DIAMOND PLATNUMZ AZINDUA PAFYUM YAKE AINA YA (CHIBU), YAINGIA RASMI KWENYE SOKO, KUPATIKANA MADUKA YOTE YA GSM

   Msanii wa muziki wa kizazi kipya,ambaye amekuwa akifanya vyema ndani na nje ya nchi (anga za Kimataifa),Naseeb Abdul a.k.a Diamond Platnumz akizungumza mbele ya Waandishi wa habari pamoja na wadau wengine waliohudhuria hafla fupi iliyohusu uzinduzi wa manukato (Pafyum) yake iliyoitwa CHIBU,mapema leo jijini Dar.
  Wakati wa uzinduzi huo Diamond alisema kuwa ameamua kuingia kwenye soko la kutengeneza manukato 'pafyum' yenye nembo yake CHIBU ili kusaidia serikali katika suala zima la kutatua changamoto ya uhaba wa ajira nchini lakini pia kuongeza pato la Taifa kwa kulipa Kodi.

  Amesema kuwa kuanza kutengenezwa na kuuzwa kwa pafyum hizo kutaongeza ajira kwa vijana wengi lakini pia kutasaidia kukuza uchumi wa nchi kupitia kodi zitakazotozwa kutokana na bidhaa hiyo ambayo wanaume na wanawake wote wanaweza kuitumia, Pafyum ya CHIBU itapatikana katika maduka yote ya GSM na itauzwa bei ya rejareja kiasi cha shilingi 105.000 kwa moja.

  Katika mkakati mwingine wa soko Meneja wa Msanii huyo Bw. Salaam Mendes amesema wako katika mazungumzo na mashirika kadhaa likiwemo shirika la ndege la Kenya Airways kwa ajili ya kuitangaza bidhaa hiyo na kuifikisha kwenye soko la kimataifa ikiwa ni pamoja na kuuzwa katika maduka makubwa kwenye viwanja vya ndege katika nchi mbalimbali ambako ndege za shirika hilo zinafika
  Msanii Nasseb Abdul a.k.a Diamond Platnumz akimkabidhi chupa ya Pafyum,mteja wake wa kwanza aliyejitambulisha kwa jina la Aisha Azori,wakati wa uzinduzi huo.Mwana mama huyo alionekana kujisikia fahari kununua bidhaa ambayo imetengenezwa na Msanii wa hapa nyumbani,ambae pia anafanya vyema katika kazi zake za Muziki,kushototo ni Mmoja wa mameneja wa Diamond Plutnamz almaarufu kwa jina la Babu Tale. 
   Msanii Diamond akifafanua jambo kwa Wanahabari
   Msanii Diamond akionesha moja ya Pafyum yake mbele ya Wanahabari na wadau mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo fupi iliofanyika jijini Dar Es Salaam mapema leo.
  Baadhi ya Wanahabari wakimsikiliza Diamond alipokuwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa Pafyum hiyo ambayo tayari imekwisha sambaza kwenye maduka mengi jijini Dar.
   Mmoja wa Meneja wa Diamond Platnumz almaarufu kwa jina la Babu Tale akiwakaribisha wana habari na wadau mbalimbali waliofika kushuhudia tukio hilo adhimu la uzinduzi wa Pafyum ya msanii huyo iliyojulikana kwa jina la CHIBU
   Diamond Platumz akiendelea kuzungumza na Wanahabari pamoja na Wadau wake waliofika kulishuhudia tukio la uzinduzi huo

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: DIAMOND PLATNUMZ AZINDUA PAFYUM YAKE AINA YA (CHIBU), YAINGIA RASMI KWENYE SOKO, KUPATIKANA MADUKA YOTE YA GSM Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top