728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Wednesday, April 12, 2017

  BOHARI YA DAWA (MSD) YAWAHAKIKISHIA WAWEKEZAJI FURSA NCHIN


  Na Mwandishi Wetu, Mwanza

  BOHARI ya Dawa (MSD) imeshiriki Jukwaa la Biashara, lililoandaliwa na Kampuni ya magazeti ya TSN,jijini Mwanza.

  Katika Jukwaa hilo,MSD pia imeshiriki maonesho ya vifaa tiba.


  Akiwasilisha mada katika jukwaa hilo jijini Mwanza jana Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Laurean Bwanakunu (pichani kulia) amewahakikishia wadau wa Mwanza fursa ya uwekezaji kwenye viwanda vya kuzalisha dawa nchini,endapo watakidhi ubora unaohitajika.

  Amesema,hatua hii inafuatia utekelezaji wa sera ya ushirikishwaji wa Sekta binafsi na taasisi za Umma katika uwekezaji.

  Bwanakunu amefafanua kuwa uanzishwaji wa viwanda nchini utapunguza gharama za uagizaji dawa na vifaa tiba toka nje ya nchi, kuokoa fedha za kununua nje,kusafirisha,kugomboa na kupata dawa kwa muda mfupi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: BOHARI YA DAWA (MSD) YAWAHAKIKISHIA WAWEKEZAJI FURSA NCHIN Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top