728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Wednesday, April 12, 2017

  Balozi Asha-Rose Migiro awasilisha hati za utambulisho kwa Rais Michael D. Higgins wa Ireland

   Balozi wa Tanzania nchini Uingereza na Ireland, Dkt Asha-Rose Migiro mapema mwezi huu aliwasilisha hati ya utambulisho (letter of credence) kwa Rais wa Ireland, Mhe. Michael D. Higgins.

  Akiwasilisha hati hiyo katika Ikulu ya Ireland, Balozi Migiro alimfikishia Rais Higgins salam za Mhe. Rais John Magufuli na wananchi wa Tanzania pamoja na kumuahidi kufanya kazi itakayoimraisha uhusiano wa kihistoria baina ya Serikali za Tanzania na Ireland pamoja na kuanzisha maeneo mapya ya ushirikiano kwa kuzingatia vipaumbele vya Serikali ya awamu ya tano ya kujenga uchumi wa viwanda. Kabla ya kuagana na Rais Higgins, Balozi Migiro alikagua gwaride rasmi liliondaliwa na kikosi cha Jeshi la Anga la nchi hiyo.  

  Akiwa Ireland, Balozi Migiro pia alikutana kwa mazungumzo na wanadiaspora wa Tanzania waishio katika miji mbalimbali ya Ireland.
  Katika mkutano huo aliwasihi wanadiaspora kushikamana, kuwa wamoja na kuunda Jumuiya ya Watanzania waishio Ireland akiwakumbusha kauli ya wahenga isimayo kuwa 'Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu'.
  Balozi wa Tanzania nchini Uingereza na Ireland, Dkt Asha-Rose Migiro  akimkabidhi Rais Michael D. Higgins hati ya utambulisho kutoka kwa Mhe.Rais John Pombe Magufuli.
  Balozi wa Tanzania nchini Uingereza na Ireland, Dkt Asha-Rose Migiro  akikagua gwaride la heshima la kikosi cha jeshi la anga la Ireland
  Balozi wa Tanzania nchini Uingereza na Ireland, Dkt Asha-Rose Migiro  akiagana na Rais Higgins.
   Michael D. Higgins akimuaga Balozi wa Tanzania nchini Uingereza na Ireland, Dkt Asha-Rose Migiro baada ya kupokea hati yake ya utambulisho 
  Balozi wa Tanzania nchini Uingereza na Ireland, Dkt Asha-Rose Migiro  alikutana kwa mazungumzo na wanadiaspora wa Tanzania waishio katika miji mbalimbali ya Ireland.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Balozi Asha-Rose Migiro awasilisha hati za utambulisho kwa Rais Michael D. Higgins wa Ireland Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top