728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Tuesday, March 28, 2017

  WAZIRI MKUU ATEMBELEA MGODI öWA BUZWAGI NA KUCHUKUA SAMPULI ZA MCHANGA

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa afanya ziara katika Mgodi wa Buzwagi 27 March 2017 kwa ajili ya kuangalia Mchanga uliowekwa katika Makontena kwa ajili yakusafirishwa nnje ya nchi katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainabu Telaki, na kushoto ni Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Bwana Stewart Hamilton
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia Sampuli ya Mchanga wenye Dhahabu unao safirishwa Nnje ya Nchi na Mgodi wa Buzwagi uliopo Kahama Mkoani Shinyanga Waziri Mkuu Alifika katika Mgodi huo 27march2017 kuangalia na kuchukua Sampuli ya Mchanga ili Serekali Ikaupime katika Maabara za Serekali
  A0227 Mtaalamu wa Madini akiweka Sampuli ya Mchanga katika Mfuko kutoka katika baadhi ya Makontena na kumkabidhi Waziri Mkuu Kassim Majaliwa nakuondoka nao kwa ajili ya kuupeleka katika Maabara ya Serekali inayo shugulika na Upimaji wa Madini Wziri Mkuu alifanya ziara katika mgodi wa Buzwagi 27March2017 kwalengo ya kujionea aina ya Mchanga unao safirishwa nnje ya Nnchi na Baadhi ya Migodi inayo Chimba Dhahabu hapa Nchini
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro katika Uwanja wa Ndege wa Mgodi wa Buzwagi 27March2017 katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainabu Telaki Viongozi hao walifika kumpokea Waziri Mkuu alipofika kuangalia shughuli za Mgodi wa Buzwagi uliopo wilaya Kahama Mkoa wa Shinyanga

  Picha zote na PMO

  …………

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefanya ziara kwenye mgodi wa dhahabu wa Buzwagi uliopo wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga na kuchukua sampuli za mchanga katika makontena mbalimbali kwa lengo la kwenda kuyapima kwa wataalamu wa madini ili kubaini kiasi cha dhahabu kilichomo.

  Amesema wanataka kuona mchanga unaosafirishwa na mwekezaji huyo unakiasi gani cha dhahabu, pia Serikali inataka kufahamu kama kodi inayolipwa ni sahihi.” Hata hivyo tayari Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli alishatoa tangazo la kuzuia usafirishaji wa michanga kwenda nje ya nchi,”.

  Waziri Mkuu alitembelea mgodi huo jana jioni (Jumatatu, Machi 27, 2017) na kuchukua sampuli za mchanga kwa lengo la kuondoa mashaka juu ya kinachosafirishwa. Sampuli hizo amezichukuwa kwenye makontena yaliyofungwa kwa ajili ya kusafirishwa kwenda nje ya nchi.

  “Tumeamua kuchukua sampuli za mchanga ambao mwekezaj anasema wanaupeleka nje ya nchi kwa ajili ya kwenda kutenganisha madini ya dhahabu na shaba. Hata hivyo nimemuhoji kwa nini mitambo hiyo isiletwe nchini ili kila kitu kifanyike hapahapa,”

  Waziri Mkuu amesema sera ya uwekezaji inasema mtambo huo unatakiwa uwepo nchini ili kila hatua ya uchenjuaji ifanyike hapa hapa, hivyo tunataka kujiridhisha na mwenendo wa mwekezaji na mapato tunayoyapata kama yanastahili.

  Aliongeza kwamba “Hili lipo miongoni mwa masharti ya uwekezaji kwenye sekta ya madini nchini kwamba mitambo hiyo ije kujengwa hapa nchini na itaongeza fursa ya ajira na kukuza sekta nyingine ikiwemo ya kilimo,”.

  Wakati huohuo Waziri Mkuu amewataka Watanzania kuwa nasubira wakati Serikali ikiendelea na zoezi la kuchunguza athari zitokanazo na kusafirisha mchanga wa madini nje ya nchi. Pia amewatoa wasiwasi wafanyakazi katika migodi na wamiliki kutowapunguza na badala yake waache waendelee na majukumu yao.

  Kwa upande wake Meneja Uendelezaji wa mgodi huo Bw. George Mkanza alisema mgodi huo ulionzishwa mwaka 2009 umeajiri watumishi 720 pamoja na vibarua 500.

  Alisema kwa siku wanachenjua makontena matatu hadi sita ambapo katika kila kontena moja wanapata kilo tatu za madini ya dhahabu na tani nne za madini ya shaba.

  Bw. Mkanza alisema wanazalisha asilimia 50 ya madini ya dhahabu na asilimia 50 ya dhahabu iko kwenye mchanga na inakuwa imechanganyika na madini ya shaba ambayo ndiyo unaosafirishwa kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kutenganishwa.

  “Hapa Buzwagi tuna makontena 179, makontena mengine 152 yako Dar es Salaam kwenye bandari kavu ya Nazam na 21 yako bandarini. Kila siku tunapoendelea kuzalisha tunakuwa na makontena manne hadi sita. Ndugu zetu wa Bulyanhulu nao wanamakontena 108 yako mgodini na 104 yako Nazam Cargo Dar es Salaam,” alisema.


  IMETOLEWA NA:

  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  L. P. 980,

  DODOMA.

  JUMANNE, MACHI 28, 2017.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: WAZIRI MKUU ATEMBELEA MGODI öWA BUZWAGI NA KUCHUKUA SAMPULI ZA MCHANGA Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top