728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Friday, March 24, 2017

  WAZIRI LWENGE AISHUKURU KUWAIT KUSAIDIA MIRADI YA MAJI NCHINI.

   Waziri  wa Maji na Umwagiliaji wa Tanzania  Gerson Lwenge ameishukuru Kuwait kwa kusaidia miradi mbalimbali ya maji inayotekelezwa hapa nchi na kueleza kuna anatarajia ushirikiano zaidi hasa katika miradi ya umwagiliaji. 

  Kupitia mikopo mbalimbali inayotolewa  na Mfuko Wa Kuwait Wa Maendeleo ya Kiuchumi kwa miradi mikubwa ya umwagiliaji. 

  Waziri Lwenge alitolea mfano wa mradi wa hivi karibuni katika mikoa ya Same na Mwanga, Kaskazini  mwa Tanzania, mradi ambao una thamani ya dola za marekani milioni 34.

  Waziri pia aligusia miradi mingine miwili  ya umwagiliaji katika  bonde la Muhongo na Luichi kaskazini-magharibi mwa Tanzania ambayo ina thamani ya dola za marekani milioni 15. 

  Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait unatarajia kutuma wataalamu wake Tanzania kwa  lengo la kutathmini miradi hii  miwili katika nusu ya kwanza ya mwaka 2018. 

   Waziri pia alitoa Pongezi na shukrani zake za dhati kwa ujumbe wa Kuwait Red Crescent Society uliofanya ziara nchini Tanzania hivi karibuni na kufungua visima 16 katika shule mbalimbali  za serikali ikiwa ni utekelezaji wa Mpango wa Kisima kwa Kila Shule.

  Ikumbukwe kuwa Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jassim Al Najema ameanzisha  mpango huo wa Kisima kwa Kila Shule kuunga mkono wito wa Rais John Magufuli wa kusaidia sekta ya elimu nchini na kukabiliana na ukame na uhaba wa maji safi ya kunywa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: WAZIRI LWENGE AISHUKURU KUWAIT KUSAIDIA MIRADI YA MAJI NCHINI. Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top