728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, March 30, 2017

  WATAALAMU WA BODI YA UNUNUZI NA UGAVI PSPTB WATOA MAFUNZO CHUO CHA (IPS) CHANIKA LEO

  Ally Songoro Mkurugenzi wa Maendeleo ya Taaluma Bodi ya Ununuzi na Ugavi(PSPTB) akitoa mada kwa wanafunzi wa Ununuzi na Ugavi katika Chuo cha (IPS) kilichopo Chanika jijini Dar es salaam. wakati wataalamu wa bodi hiyo walipotoa mafunzo ya taaluma hiyo katika chuo hicho, Bw. Ally Songoro amehimiza kufuatwa kwa maadili wakati wa kutekeleza majukumu yao ambapo unatakiwa umakini mkubwa huku wakifuata maadili, Kanuni na taratibu za ununuzi na ugavi wakati watakapokuwa katika ajira zao kwenye taasisi mbalimbali hapa nchini na kwingineko.
  Baadhi ya wanafunzi hao wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa na wataalamu kutoka Bodi ya ununuzi na ugavi (PSPTB) kwenye chuo hicho.
  Mmoja wa wakufunzi wa chuo hicho akiwaeleza jambo wanafunzi hao wakati alipokuwa akiwakaribisha wataalamu kutoka Bodi ya Ununuzi na Ugavi (PSPTB) ili kutoa mafunzo kwa wanafunzi hao.
  Shamim Mdee Afisa Mwandamizi wa Masoko na Mahusiano ya Umma(PSPTB) akizungumza jambo na wanafunzi wa taaluma ya Ununuzi na Ugavi katika chuo cha (IPS) Chanika jijini Dar es salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: WATAALAMU WA BODI YA UNUNUZI NA UGAVI PSPTB WATOA MAFUNZO CHUO CHA (IPS) CHANIKA LEO Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top