728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, March 16, 2017

  WADAU WA ZAO LA MKONGE WAFANYA MKUTANO SHINYANGA


  Alhamis ,Machi 16,2017 kumefanyika Mkutano wa wadau wa zao la mkonge kutoka wilaya ya Meatu mkoa wa Simiyu na wilaya ya Kishapu mkoa wa Shinyanga. 

  Mgeni rasmi katika mkutano huo ulioandaliwa na shirika la OXFAM na asasi isiyo ya kiserikali inayojishughulisha na Maendeleo ya Jamii (Relief to Development Society- REDESO) alikuwa mkuu wa wilaya ya Kishapu mheshimiwa Nyabaganga Talaba.

  Awali akizungumza katika mkutano huo,Mratibu Miradi (uchumi) kutoka shirika la OXFAM Haji Kihwele alisema lengo la mkutano huo kuwaweka pamoja wadau hao ili waweze kufahamiana sambamba na kujadili namna ya kulifanya zao hilo kuwa na tija na manufaa zaidi kwa wakulima na kuwasaidia wakulima hao kupata masoko. "Tumekutana hapa ili tujadili pia namna ya kumuunganisha mkulima wa mkonge anufaike na masoko yenye faida na kupata uwakilishi mzuri katika sekta hii",alisema Kihwele. 

  Akizungumza katika mkutano huo,mkuu wa wilaya ya Kishapu mheshimiwa Nyabaganga Talaba aliwataka wadau wa zao la mkonge kwenda kuwekeza kwa kujenga viwanda katika wilaya yake kwani ardhi ipo ya kutosha. 

  "Wadau wa mkonge njooni Kishapu muwekeze,tunayo ardhi ya kutosha,hivi sasa maji kutoka ziwa Victoria yamefika Kishapu,umeme na barabara zinazopitika kipindi chote zipo,tunataka kulifanya zao la mkonge kuwa rasmi badala ya kutumika kwenye mipaka kutenganisha mashamba na milingoti kwa ajili ya kujengea nyumba",alieleza Nyabaganga. 

  "Kipindi cha majaribio kimekwisha,tunalima pamba lakini pia tumeamua kulima mkonge,tunataka kilimo hiki kiwe rasmi,wananchi wanajitahidi kulima zao la mkonge lakini changamoto kubwa iliyopo ni ukosefu wa soko hivyo ni vyema ofisi za bodi ya mkonge zikawa na ofisi katika maeneo yanayolima,wakulima wanahitaji kunyanyuliwa kwani hata mikopo inayotolewa haitoshi",aliongeza Nyabaganga. 

  Miongoni mwa wadau walioshiriki katika mkutano huo ni wakulima na wasindikaji wa zao la mkonge,wazalishaji wa bidhaa za mkonge,taasisi za kifedha ikiwemo Vision Fund,bodi ya mkonge (TSB),Chemba ya wafanyabiashara,wakulima na viwanda (TTCIA),Shirika la kuhudumia viwanda vidogo (SIDO),Umoja wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA),Mtandao wa Asasi za Wakulima (Agriculture Non- State Actors Forum -ANSAF) na viongozi mbalimbali kutoka halmashauri ya wilaya ya Kishapu na Meatu. 
  Mratibu Miradi (uchumi) kutoka shirika la OXFAM Haji Kihwele akizungumza wakati wa mkutano wa wadau wa zao la mkonge uliofanyika katika ukumbi wa Virgimark Hotel mjini Shinyanga leo Alhamis Machi 16,2017-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog 
  Wadau wa zao la mkonge wakimsikiliza Mratibu Miradi Kiuchumi kutoka OXFAM Haji Kihwele 
  Meneja Mradi wa asasi isiyo ya kiserikali inayojishughulisha na maendeleo ya jamii (Relief to Development Society- REDESO) Charles Buregeya akizungumza katika mkutano wa wadau wa zao la mkonge kutok wilaya ya Kishapu na Meatu 
  Mkuu wa wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga mheshimiwa Nyabaganga Talaba akizungumza wakati wa mkutano huo 
  Washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Kishapu mheshimiwa Nyabaganga Talaba 
  Mkuu wa wilaya ya Kishapu mheshimiwa Nyabaganga Talaba akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa zao la mkonge kutoka wilaya ya Meatu na Kishapu 
  Mkuu wa wilaya ya Kishapu mheshimiwa Nyabaganga Talaba akizungumza ukumbini 
  Mkuu wa wilaya ya Kishapu mheshimiwa Nyabaganga Talaba akizungumza ukumbini ambapo alisema serikali imedhamiria kuanzisha viwanda na kwamba kinachotakiwa ni kuwa tayari kuzalisha zao la mkonge.Kulia ni kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu George Kessy
  Kulia ni Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu Boniphace Butondo na Afisa Biashara halmashauri ya wilaya ya Kishapu Konisaga Mwafongo 
  Mratibu wa Miradi (Ardhi) kutoka OXFAM bi Amina Ndiko akisisitiza jambo kwenye mkutano huo 
  Meneja Mradi REDESO Charles Buregeya (kushoto) na Mratibu Miradi (uchumi) shirika la OXFAM Haji Kihwele 
  Mratibu wa Miradi (Ardhi) kutoka OXFAM bi Amina Ndiko akizungumza ukumbini 
  Washiriki wa mkutano huo wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini 
  Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu Boniphace Butondo akichangia hoja katika mkutano wa wadau wa zao la mkonge 
  Mwakilishi wa Shirikisho la Wakulima na Wasindikaji wa zao la mkonge wilaya ya Kishapu( SHIWAKI),Yusuph Mboje akielezea kuhusu kazi zinazofanywa na shirikisho hilo lililoanzishwa mwaka 2016 ambalo linakabiliwa na changamoto ya kukosa soko la mkonge na kukosekana kwa mkataba na mnunuzi wa kudumu wa zao hilo 
  Mwakilishi wa akina mama wanaojishughulisha na kilimo cha mkonge Anastazia Christopher kutoka Kishapu akielezea faida wanazozipata kupitia kilimo cha mkonge ambazo ni pamoja kuacha kuwa tegemezi kwa waume zao,kusomesha watoto n.k 
  Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu Boniphace Butondo na mkuu wa wilaya ya Kishapu Nyabaganga Talaba wakiwa ukumbini 
  Mratibu wa Miradi (Ardhi) kutoka OXFAM bi Amina Ndiko akiongezea maelezo kutoka kwa akina mama kutoka Kishapu wanaolima mkonge 
  Mkulima wa zao la mkonge kutoka Kishapu Fredina Said akimuonesha mkuu wa wilaya ya Shinyanga Nyabaganga Talaba zulia lililotengenezwa kwa mkonge 
  Mraghbishi kutoka Taasisi ya Kuimarisha Demokrasia na Utawala Bora (ADLG) ambaye pia ni Mwakilishi wa Mtandao wa Asasi za Wakulima (Agriculture Non- State Actors Forum -ANSAF) bwana Nicholaus Luhende Ngelela akizungumza kwenye mkutano huo ambapo alisisitiza umuhimu wa wakulima wa zao la mkonge kuunda mtandao wao 
  Katibu mtendaji Chemba ya wafanyabiashara,wakulima na viwanda (TTCIA) mkoa wa Mwanza Hassan Karambi akizungumza ukumbini 
  Taasisi isiyo ya kiserikali yenye kusaidia sekta ya kilimo (Private Agricultural Sector Support - PASS) Emilian Barongo akizungumza ukumbini 


  Jeremiah Maleko kutoka Vision Fund akieleza namna wanavyotoa mikopo kwa wakulima
  Afisa udhibiti Ubora kutoka Bodi ya Mkonge Olivo Mtunge akielezea kuhusu hali ya soko la mkonge hivi sasa na fursa za mkulima mdogo ili aweze kunufaika na kilimo hicho
  Picha ya pamoja washiriki wa mkutano wa wadau wa zao la mkonge kutoka wilaya ya Meatu na Kishapu
  Picha ya pamoja washiriki wa mkutano huo .Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: WADAU WA ZAO LA MKONGE WAFANYA MKUTANO SHINYANGA Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top