728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Monday, March 27, 2017

  VIONGOZI WA DINI WAJITOKEZA KUMPONGEZA RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI.   Askofu wa Kanisa la Good news Minstry Dk. Charles Gadi akizungumza na waandishi wa habari juu ya kumpongeza Rais Dk.John Pombe Magufuli leo jijini Dar es Salaam.

  Askofu wa Kanisa la Good news Minstry Dk. Charles Gadi amempongeza Rais Dk.Jonh Pombe Magufuli kwa hatua yakuzuia mchanga uliokuwa wanataka kusafirisha nje ya nchi ilikuweza kuchakata dhahabu .

  Akizungumza na waandishi wahabari jijini Dar es salaam Askofu Gadi amesema kuwa kusafirisha mchanga wa`madini ya dhahau ni sawana kuiuza Tanzania nje ya nchi.

  Amesema kuwa Rais Dk. John Pombe Magufuli amekuwa mtu wa kuthubutu kuona nchi ya Tanzania inakuwa ya maendeleo na wananchi baada wataona mafanikio hayo.

  Gadi amesema kuwa wakiwa viongozi wa dini wanajibu wa kumuombea Rais Dk. John Pombe Magufuli kuwa Tanzania ifanikiwe kutokana na harakati zake. Aidha wa amesema kuwa Tanzania ya viwanda inawezekana kutokana na Rais kuweka kipaumbele kwa wawekezaji ili Tanzania kuingia katika rekodi ya uchumi wa kati .
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: VIONGOZI WA DINI WAJITOKEZA KUMPONGEZA RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI. Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top