728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, March 30, 2017

  UWT YAIPONGEZA KAMATI KUU YA CCM,YAWAHAMASISHA WANACHAMA WAKE WENYE SIFA KUJITOKEZA KWA WINGI KUGOMBEA NAFASI MBALIMBALI ZA UONGOZI

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania UWT, Amina Makilagi akizungumza na waandishi wa habari, leo, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam.

  Bi Makilagi alizungumza mambo mbalimbali ikiwemo na kutoa pongezi nyingi kwa Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM ikiongozwa na Mwenyekiti wake,Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa uamuzi wake wa kuteua wagombea wa Ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki kwa uwiano ulio sawa baina ya Wanaume na Wanawake.

  Bi Makilaki amesema kuwa UWT inawahamasisha Wanachama wake wana CCM wenye sifa kujitokeza kwa wingi  kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa ndani wa chama na Jumuiya zake ambapo kwa UWT Uchaguzi wa ngazi ya Tawi utaanza April mosi mpaka 10/2017.

  Taarifa zaidi hii hapa chini.  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: UWT YAIPONGEZA KAMATI KUU YA CCM,YAWAHAMASISHA WANACHAMA WAKE WENYE SIFA KUJITOKEZA KWA WINGI KUGOMBEA NAFASI MBALIMBALI ZA UONGOZI Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top