728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Wednesday, March 15, 2017

  Tanzania katika Mkutano wa 61 wa Kimataifa wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York, Marekani

   Mheshimiwa Dkt. Hamisi Kigwangalla (Mb) , Naibu Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto akichangia mada katika kikao cha ngazi  ya Mawaziri kuhusu uwezeshaji wa Wanawake Waliopo kwenye sekta isiyo rasmi.

  Dkt. Kigwangalla ameelezea jinsi ambavyo kwa upande wa Tanzania, Serikali imepiga jitihada Kubwa kuhakikisha inamkomboa mwanamke kutoka kwenye utegemezi kwa kuunda vyombo mbalimbali na kuandaa sera na miongozo inayoelekeza usawa katika kufikia malengo ya kumkomboa mwanamke kiuchumi ambapo mwanamke anakuwa na haki na uwezo wa kukopa katika taasisi mbalimbali ili kuanzisha au kukuza mtaji wa biashara yake katika kufikia malengo aliyotarajia. 

  Vile vile amesema serikali imeanzisha mfuko wa maendeleo katika halmashauri zote 114 nchini ili kuwafikia wanawake walio wengi zaidi , imeendelea kuhamasisha Jamii kuanzisha  mifuko mbalimbali ya kuweka na kukopa Kama vile (VIKOBA)  , kuwahamasisha kushiriki katika maonyesho mbalimbali ya kitaifa na hata mikutano mikubwa ya kimataifa ili kujitangaza na kukuza bidhaa mbalimbali kwa lengo la kujipatia kipato na kukuza mitaji yao.

  Alisema, katika kufanya hivyo, kunawasaidia kutengeneza mitandao ya kibiashara itakayowasaidia kukua kimataifa na kufanya biashara Kubwa za kimataifa na pia kutoa ajira kwa Wanawake wenzao . Pia , Serikali imeanzisha benki ya Wanawake ambayo Kazi yake Kubwa ni kutoa mikopo na ushauri ambao utawasaidia  kukuza biashara zao na kuongeza kipato kwani Wanawake ni Jeshi Kubwa ambalo linachangia uchumi wa nchi kwa kiasi kikubwa.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Tanzania katika Mkutano wa 61 wa Kimataifa wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York, Marekani Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top