728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Friday, March 24, 2017

  SPIKA WA BUNGE AFUNGUA MKUTANO WA KAMATI TENDAJI YA CPA KANDA YA AFRIKA.

  Katibu Msaidizi wa Chama cha Mabunge Wanachama Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika (CPA Africa Region ) Bw. Demetrius Mgalami akimuelezea jambo Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai kabla ya kuanza kwa Mkutano wa 72 wa Kamati Tendaji ya CPA Afrika Jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Afrika kusini Mhe Lindiwe Maseko ( wa pili kushoto) na Katibu wa Chama cha  CPA Afrika ambaye pia ni Katibu wa Bunge la Tanzania   Dkt Thomas Kashililah.
   Wajumbe wa Kamati Tendaji ya CPA Afrika  wakiimba wimbo wa Jumuiya hiyo kabla ya kuanza kwa Mkutano huo.
  Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Wajumbe wa Kamati Tendaji CPA Afrika  wakati wa Mkutano wa Chama hicho uliofanyika Jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Viongozi wa Kamati hiyo.
  Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya CPA Afrika ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Afrika Kusini Mhe. Lindiwe Maseko akizungumza wakati wa Mkutano huo.
  Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai (kulia waliokaa mbele) ambaye pia ni Mwenyejiti wa Bodi ya Chama cha CPA Afrika akiongoza kikao cha Bodi hiyo mara baada ya kikao cha Kamati Tendaji ya chama hicho kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya CPA Mhe. Lindiwe Maseko. Wengine katika picha ni Wajumbe wa Bodi hiyo.(Picha na Ofisi ya Bunge).                                              
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: SPIKA WA BUNGE AFUNGUA MKUTANO WA KAMATI TENDAJI YA CPA KANDA YA AFRIKA. Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top