728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Friday, March 17, 2017

  RIDHIWANI:NASHUKURU KWA KUHOJIWA NA MAMLAKA YA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA, ASEMA JAMII SASA IMEJUA UKWELI WA JAMBO HILO

  Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete ameeleza kufurahishwa kwake baada ya kuhojiwa na Mamlaka ya kuzuia na Kupambana na Dawa za kulevya nchini.
  Mbunge huyo amezungumza hayo  jijini Dar es salaam baada ya kuhojiwa na Mamlaka hiyo, ambapo alisema roho yake imesuuzika kwani jamii imeamini kwamba hahusiki kwa namna yoyote ile na biashara hiyo haramu.
  "nashukuru kwa kuhojiwa huku nimepata nafasi ya kueleza ukweli juu ya jambo hili ambalo lilishaanza kuleta taharuki katika jamii, sasa umma umejua kuwa siuzi wala sihusiki na dawa za kulevya roho yangu imesuuzika "alisema Ridhiwani
  Alisema vita ya dawa ya kulevya ni kubwa na inapaswa kupigwa na kila mmoja ili kuokoa kundi kubwa la vijana ambao wanaathirika kutokana na suala hilo na kwamba kuhojiwa kwake kumemfanya awe na amani.
  Msikilize hapa:
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: RIDHIWANI:NASHUKURU KWA KUHOJIWA NA MAMLAKA YA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA, ASEMA JAMII SASA IMEJUA UKWELI WA JAMBO HILO Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top