728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Monday, March 27, 2017

  REPOA-TANZANIA IPO KATIKA MWENENDO MZURI WA MAENDELEO YA VIWANDA

  Mkurugenzi Mtendaji  wa REPOA Tanzania  Dkt. Donald Mmari, akizungumza na waandishi wa habari juu Semina juu ya Maendeleo ya Viwanda nchini
   Waandishi wakiwa katika mkutano huo wakisikiliza kwa makini

   Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii

  Tanzania imeonekana kuwa katika mwenendo mzuri katika mageuzi ya viwanda na kuanza kufanya vizuri katika sekta hiyo kutokana na usimamizi wa Serikali.

  Hayo yamesemwa mapema leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji  wa REPOA nchini, Dkt. Donald Mmari alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya Semina itakayofanyika March 29 na 30 jijini Dar es Salaam itayohusu umuhimu wa taasisi katika maendeleo ya Viwanda nchini.

  "Kuna muelekeo mzuri sana katika juhudi za ukuzaji Viwanda nchini, kwani kwa sasa mazingira ni mazuri tofauti na hapo awali,nchi yetu ina umeme wa uhakika jambo ambalo ni la kwanza katika uchumi wa Viwanda" amesema  Dkt. Mmari

  Amesema kuwa katika semina hiyo kwa mwaka huu kutakuwa na msemaji kutoka nchini Canada, ambaye ataeleza ni kwa jinsi gani wao wamefanikiwa katika sekta ya Viwanda.

  Pia ametaja kuwa wadau wote watakuwa na ajenda moja tu inayofanana kwa ajili ya kusaidia kukua kwa sera ya viwanda ili nchi iweze kupiga hatua.
  Dkt. Alfred Kinyondo akifafanua jambo mbeke ya waandishi wa habari

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: REPOA-TANZANIA IPO KATIKA MWENENDO MZURI WA MAENDELEO YA VIWANDA Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top