728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Wednesday, March 15, 2017

  RC PAUL MAKONDA ATIMIZA MWAKA MMOJA SASA,AZUNGUMZA NA KULA NA WAATHIRIKA WA DAWA ZA KULEVYA

  Mkuu wa Mkoa Paul Makonda akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali,wakiwemo Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa jiji la Dar,viongozi wa Dini mbalimbali,Wasaniii na vijana kutoka vituo mbalimbali vya matibabu ya dawa za kulevya walijitokeza kumsikiliza RC Paul Makonda ambaye leo alikuwa anatimiza mwaka wake mmoja wa Uongozi tangu aapishwe na Rais wa awamu ya tano,Dkt John Pombe Magufuli.
  Baadhi ya waathirika wa Madawa ya Kulevya wapato zaidi ya 1500 kutoka vituo mbalimbali vinavyotoa matibabu ya Dawa za kulevya,wakiwa ndani ya bwalo la Polisi Oysterbay jijini Dar,wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa Paul Makonda alipokuwa akizungumza nao mambo mbalimbali,ya kimaendeleo pamoja na kupewa elimu mbalimbali ihusuyo dawa za kulevya.RC Makonda leo anatimiza mwaka mmoja tangu aapishwe kuwa mkuu wa mkoa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli,
  Baadhi ya Viongozi mbalimbali wa dini,walialikwa kwenye hafla hiyo fupi ya kutimiza mwaka mmoja kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar,Paul Makonda
  Pichani ni baadhi ya wasanii walioshiriki na kutoa neno katika hafla hiyo,wasanii hao ni TID,Diamond Paltnumz,Harmonize,Banana Zorro,Mrisho Mpoto na wengineo ambao walijitokeza kumuunga mkono RC Makonda katika suala zima la kupambana na Dawa 
  za kulevya.
  Vijana waliothiriwa na Madawa ya kulevya ambao kwa sasa wameahidi kuacha kutumia wakiwa wameandika bango lao la kumshukuru RC Makonda kwa kazi yake nzuri aifanyayo ya kupambana na Dawa za Kulevya.
  Vijana mbalimbali walikokuwa wakitumia dawa za kulevya wakimshukuru RC Makonda kwa juhudi zake kubwa za kuhakikisha dawa za kulevya zinatokea ndani ya jiji la Dar kwa namna moja ama nyingine
   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: RC PAUL MAKONDA ATIMIZA MWAKA MMOJA SASA,AZUNGUMZA NA KULA NA WAATHIRIKA WA DAWA ZA KULEVYA Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top