728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Friday, March 17, 2017

  RC NDIKILO ,RIDHIWANI, BHARWANI WAUNGA MKONO UJENZI WA MADARASA S/M VIGWAZA

  Katibu wa Mbunge Ridhiwani Kikwete, bw. Iddi Swala akizungumza na wakazi wa kijiji cha Vigwaza kuhusu utekelezaji wa mfuko wa jimbo na Ridhiwani alivyosaidia kijiji hicho na kata kijumla. (picha na Mwamvua Mwinyi)

  Katibu wa mbunge wa Ridhiwani Kikwete, anaeitwa Iddi Swala akionyesha saruji waliochangia ujenzi wa shule ya msingi Vigwaza. (picha na Mwamvua Mwinyi)  Mifuko 50 ya saruji iliyochangiwa na mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete, na mifuko 50 aliyochangia diwani wa kata ya Vigwaza Mohsin Bharwani kwa ajili ya ujenzi wa madarasa sita shule ya msingi Vigwaza. (Picha na Mwamvua Mwinyi)

  ………………………………………………………………

  Na Mwamvua Mwinyi,Vigwaza

  WAKAZI wa kijiji cha Vigwaza,Kata ya Vigwaza,jimbo la Chalinze,wameanza kuchangia matofali matano kila mmoja na kujitolea nguvu kazi ili kujenga vyumba vitano vya madarasa na chumba kimoja cha chekechea katika shule ya msingi Vigwaza.

  Mwenyekiti wa kijiji hicho, Ramadhani Kirumbi, alisema serikali ya kijiji imekubaliana na wananchi kuongeza majengo shuleni hapo.

  Kutokana na juhudi hizo, mkuu wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo, alieleza anatambua jitihada za wananchi hivyo atawaunga mkono kwa kuchangia sh. Mil mbili.

  Mhandisi Ndikilo, alisema jamii ishirikiane na serikali kwa kutatua changamoto za kijamii hasa elimu ili kuwajengea mazingira bora wanafunzi.

  “Tulijikita kwenye kuondoa matatizo ya uhaba wa madawati lakini kwasasa haina budi tujiongeze kumaliza changamoto ya majengo na madarasa “alibainisha .

  Nae mbunge wa jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete, alichangia mifuko ya saruji 50 na mabati 50 yenye thamani ya mil. 1.9 .

  Katibu wa mbunge huyo Iddi Swala,alisema Ridhiwani amechangia pia zahanati ya kijiji kipya cha Mnindi mifuko 50,ukarabati nyumba ya mwalimu shule ya msingi Mnindi mifuko 30.

  Hata hivyo, Ridhiwani alitoa mifuko mingine 30 kwa ajili ya kufanya ukarabati zahanati ya Kitonga.

  Katibu Swala, alieleza kwamba, mh mbunge kapeleka mifuko ya saruji mingine 50 katika shule ya msingi Milo na zahanati ya Buyuni ametoa mifuko 30 ya saruji.

  “Kati ya fedha za jimbo mil 48 kata ya Vigwaza imechangiwa mil. tano “alisema Swala kwa niaba ya Ridhiwani.

  Diwani wa kata Vigwaza,Mohsin Bharwani, alitoa mifuko 50 ya saruji na taasisi ya lions Dar es salaam -Panorama imesaidia mifuko ya saruji 50.

  Bharwani alisema kwasasa, katika sekta ya elimu wanajikita kumaliza tatizo la upungufu wa madarasa kwenye shule mbalimbali.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: RC NDIKILO ,RIDHIWANI, BHARWANI WAUNGA MKONO UJENZI WA MADARASA S/M VIGWAZA Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top