728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, March 9, 2017

  RC MASENZA AWAONYA WAZAZI KUACHA KUTUMA WATOTO USIKU WALA KUWALAZA WAGENI CHUMBA KIMOJA NA WATOTO


  Mkurugenzi wa asasi isiyo ya kiserikali ya R.D.O ambayo inajihusisha na huduma za kijamii wilaya ya Mufindi na Kilolo Fidelis Filipatali akimkabidhi mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza zawadi ya keki
  Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akiwa katika picha ya pamoja na watenda kazi wa R.D.O

  Filipatali akimkabidhi keki mkuu wa mkoa Masenza kwa ajili ya katibu tawala wa Iringa

  Wanawake wakiwa na furaha tele


  Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza kulia na mwenyekiti wa UWT Mufindi Marcelina Mkini wakichota maji

  Diwani wa kata ya Mdabulo akiwa amebebwa juu juu na wanawake baada ya diwani huyo kuimba shairi lenye mvuto kwa wanawake
  Mkurugenzi wa R.D.O Bw Filipatali kulia akiuongoza msafara wa mkuu wa mkoa wa Iringa

  Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akiwahutubia wanawake

  Katibu wa CCM wilaya ya Mufindi Jimson Mhagama kulia na mwenyekiti wa UWT Mufindi Marcelina Mkini na mratibu wa wanawake mkoa wa Iringa mama Sanga wakifuatilia hotuba ya mkuu wa mkoa
  Watumishi ofisi ya RC Iringa wakitoa zawadi kwa ajili ya Yatima
  Wasanii wa Ibwanzi wakiigiza kama Rais
  Mkuu wa mkoa akitembelea banda ya benki ya Mucoba  Mkuu wa mkoa akipokea risala ya R.D.O

  Kazi zinazofanywa na wanafunzi wa R.D.O

  Mwenyekiti wa sherehe za wanawake Mufindi

  Wafanyakazi ofisi ya mkuu wa mkoa wakiingia kwa maandamano
  Wanafunzi wa sekondari ya Mdabulo wakicheza igizo la unyanyasaji wa mwanamke

  Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akitoa msaada kwa yatima wanaolelewa na R.D.O


  Wafanyakazi ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa wakitoa misaada yao kwa yatima

  Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza na mwenyekiti wa UWT Marcelina Mkini ambae ni mjumbe wa NEC Taifa kutoka wilaya ya Mufindi wakimtwisha ndoo ya maji mmoja kati ya wanawake wakazi wa Ikanga kata ya Mdabulo wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji uliofadhiliwa na RDO  Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akiwa na wa wafanyakazi wa RDO na viongozi wa wilaya ya Mufindi mara baada ya kumalizika kwa sherehe za siku ya wanawake duniani

  Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza kushoto na mwenyekiti wa UWT Mufindi Marcelina Mkini wakiongoza maandamano ya wananchi Ikanga kata ya Mdabulo  Wanawake kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa  Na MatukiodaimaBlog

  MKUU wa mkoa wa Iringa Amina Masenza awataka wananchi mkoani hapa kutowaruhusu wageni kulala na watoto chumba kimoja.

  Kuwa kuanzia sasa mgeni akifika nyumbani kwako apewe godoro na kulala sebuleni na sio kushusha watoto vitandani na kumpa heshima mgeni Kulala kitandani chumba cha watoto.


  Mkuu huyo wa mkoa ametoa ushauri huo leo wakati akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Ikanga kata ya Mdabulo wilayani Mufindi ambako maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yalifanyika kwa mkoa wa Iringa.

  Alisema kuwa hatua kuwapa vitanda vya ama wageni kuchanganywa chumba kimoja na watoto baadhi yao si wema wapo kwa ajili ya kuwabaka watoto hao"

  Pia aliwataka wazazi kutowatuma watoto nyakati za usiku madukani ama nje ya nyumba zao kwani kuendelea kuwatuma watoto hao usiku ni kuwahatarishia usalama wao na wabakaji

  Alitaka ikifika usiku wazazi wenyewe mama na baba ndio watumane dukani kama hakuna mtu mzima wa kutumwa na sio mtoto mdogo

  Katika hatua nyingine mkuu huyo wa mkoa amepongeza taasisi isiyo ya Kiserikali ya RDO inayojishughulisha na huduma mbali mbali za kijamii wilayani Mufindi ikiwemo ya maji na malezi ya yatima.

  Pamoja na kuishukuru taasisi hiyo ya RDO chini ya mkurugenzi wake Fidelis Filipatali, bado aliwaonya baadhi ya wanasiasa wanaotaka kukwamisha mradi wa maji kwa kuingiza siasa.

  Kuwa mradi huo wa maji hauna siasa na kuwa wananchi wanahitaji maji na sio siasa na kuahidi kuendelea kuwa karibu na asasi hiyo ya RDO.

  Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Mufindi Marcelina Mkina ambae mjumbe wa NEC Taifa kutoka wilaya ya Mufindi na katibu wa CCM wilaya ya Mufindi walimpongeza Rais Dkt John Magufuli kwa kumteua Masenza kuwa mkuu wa mkoa wa Iringa na kuwa maendeleo na ushirikiano mkubwa wa serikali na chama umefanikisha maendeleo Kwa wananchi.

  Mkini alisema kuwa pongezi za utendaji kazi wa mkuu huyo wa mkoa atazifikisha rasmi kwenye mkutano mkuu wa CCM .

  Hata hivyo alipongeza mapambano dhidi ya dawa za kulevya yanayofanya na serikali ya awamu ya tano pamoja na Vita dhidi ya ufisadi na rushwa na kuwa wao UWT na CCM wapo pamoja na Rais
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: RC MASENZA AWAONYA WAZAZI KUACHA KUTUMA WATOTO USIKU WALA KUWALAZA WAGENI CHUMBA KIMOJA NA WATOTO Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top