728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Wednesday, March 15, 2017

  NAIBU MEYA TEMEKE AAGIZA SOKO LA STERIO APEWE MZABUNI

  Na Humphrey Shao, Globu ya jamii

  Naibu Meya wa Manispaa ya Temeke, Feysal Salum, ameagiza kuanzia sasa Soko la Matunda la Temeke Sterio kupewa mzabuni wa ukusanyaji mapato ili kuongeza ufanisi katika mapato ya Halmashauri.

  Salum ametoa agizo hilo mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa kujifunza kazi kwa maofisa masoko wa Halmashauri ya Wilaya ya Temeke na Madiwani, ambao walikwenda kujifunza namna jinsi gani halmashauri ya Ilala imeweza kufanikiwa kupata mapato kupitia masoko kupewa wazabuni kukusanya masoko.

  “lazima niwaambie ukweli kuwa soko hili tunalipeleka kwa wazabuni,ili tuweze kupata mapato, haiwezekani kukusanya mapato milioni 50 kwa mwezi na gharama za uzalishaji kuwa juu ya hiyo fedha, hivyo hapa hakuna namna lazima tuligawe hili soko ili tuweze kupata faida” amesema Salum.

  Amesema kuwa kwa ziadi ya miaka mitano soko hilo lilikuwa likiendeshwa kwa hasara kwa fedha kutoka Halmashauri, hivyo kuanzia sasa imefikia tamati .

  Kwa upande wake Naibu Meya Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto amewataka wanasiasa kuacha kukumbatia wafanyabiashara ambao wamekuwa wakiwaletea jeuri maofisa masoko na wakusanya ushuru kwa sababu wanafahamiana na viongozi.

  Ametaja kuwa kama viongozi wa juu watakuwa mstari wa mbele kusimamia makusanyo bila ya kumwangalia mtu wataweza kufanikiwa katika mfumo huo wa ukusanyaji kupitia mzabuni ambao una manufaa makubwa sana kwa Halmashauri.
  Naibu Meya wa Manispaa ya Temeke Faysal Salum akitoa maagizo ya soko la Sterio kupewa mzabuni mara baada ya kumalizika kwa kikao cha mafunzo kutoka kwa watendaji wa Manispaa ya Ilala
  Baadhi ya Madiwani na Watendaji kutoka Temeke wakisikiliza kwa makini maelekezo kutoka kwa Naibu Meya wa Manispaa ya Temeke.
  Naibu Meya Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto akizungumza katika kikao hicho cha madiwani na maofisa masoko kutoka Temeke na Ilala.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: NAIBU MEYA TEMEKE AAGIZA SOKO LA STERIO APEWE MZABUNI Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top