728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Sunday, March 26, 2017

  MWANAHABARI GEORGE BINAGI NA MISS PENDO KISAKA KUUAGA UKAPELA HII LEO.

  Mwanahabari wa 102.5 Lake Fm Mwanza na mwanablogu wa mtandao wa Binagi Media Group, George Binagi (kulia) pamoja na Miss Pendo Kisaka (kushoto), wanatarajiwa kufunga pingu za maisha masaa machache yajao.

  Wapendanao hao wanafunga ndoa hii leo March 26,2017 majira ya saa nane mchana katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza chini ya Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hilo, Dkt.Daniel Moses Kulola, na baadae kufuatiwa na hafla itakayofanyika Ukumbi wa Sun City Hotel uliopo Ghana Green View Jijini Mwanza kuanzia majira ya saa moja jioni.

  Zifuatazo ni picha za hafla ya kumuaga bibi harusi mtarajiwa (Sendoff) iliyofanyika ijumaa iliyopita March 17,2017 Jijini Dar es salaam.
  Sifa na Utukufu ni kwa Mwenyezi Mungu, Amina!
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: MWANAHABARI GEORGE BINAGI NA MISS PENDO KISAKA KUUAGA UKAPELA HII LEO. Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top