728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, March 16, 2017

  Msifungishe ndoa bila ya kuona vyeti vya kuzaliwa vya wahusika

   Waziri wa Mambo ya Katiba Na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe ameagiza kuwa kuanzia tarehe 1 Mei, 2017  ndoa zote zifungwe baada ya wanaotaka kufunga kuwasilisha kwa vyeti vya kuzaliwa kwanza. 

  Hivyo, amewataka wananchi wote wanaotarajia kufunga ndoa waanze kutafuta vyeti vya kuzaliwa mapema kwa sababu hawataweza kufunga ndoa kuanzia tarehe 1 Mei, 2017. 

  Agizo hilo amelitoa kwa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) leo tarehe 16/3/2017 akiwa ziarani mkoani Morogoro kukagua utendaji wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Msifungishe ndoa bila ya kuona vyeti vya kuzaliwa vya wahusika Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top