728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Tuesday, March 14, 2017

  MKUU WA MKOA WA MBEYA AWAOMBA VIONGOZI WA DINI NA MILA KUWAEPUSHA WANANCHI NA IMANI ZA KISHIRIKINA NA KUFUFUA WATU

   Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akizungumza na viongozi wa Dini, wa mitaa na wa mila katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa mkapa leo jijini mbeya
   Baadhi ya viongozi wa dini na serikali za mitaa na mila wakiwa katika ukumbi wa mkapa kumsikiliza mkuu wa mkoa wa mbeya Mh.Amos Makalla.
  Mkuu wa mkoa wa mbeya Amos Makalla watatu kutoka shoto pamoja na mkuu wa wilaya ya mbeya mh.William Ntinika wa kwanza kushoto katika picha ya Pamoja na viongozi wa Dini mkoa wa Mbeya.  Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makala  ameitisha kikao na viongozi Dini na mila kwaomba msaada wa kukemea vitendo vya kishirikina katika mkoa huo.Makala amesema hayo katika kikao chake na Viongozi wa Dini Mila na wenyeviti wa mitaa na vijiji katika mkoa wa Mbeya.

  " matukio ya watu kufukua maiti au kutozika kwa imani ya kuwafuafua  hayapaswi kuachwa yaendelee , bibilia na Quruan imeandikwa kuna kufufuliwa, kuna kiama ,kuna pepo ni baada ya kufa nawaomba  mnisaidie   kutoa Elimu na mafundisho yenye kuondosha matukio hayo" Aamesema Makala.

   Makala awaomba pia kusaidia serikali katika mapambano ya Dawa ya Kulevya kwa kutoa Elimu na hamasa ya kuelimisha madhara ya dawa ya kulevya.

  Amesema Mbeya itangazwe kwa sifa nzuri kama Mkoa unaotegemewa kwa uzalishali wa Chakula, Mkoa wa tatu kitaifa kuchangia pato la Taifa na ni Mkoa unapiga hatua kubwa kimaendeleo
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: MKUU WA MKOA WA MBEYA AWAOMBA VIONGOZI WA DINI NA MILA KUWAEPUSHA WANANCHI NA IMANI ZA KISHIRIKINA NA KUFUFUA WATU Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top