728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Saturday, March 18, 2017

  MASHA ATENGUA USHIRIKI WAKE TLS,AAMUA KUMUUNGA MKONO MGOMBEA MWENZAKE TUNDU LISSU

  Mgombea wa kiti cha urais  wa Chama cha wanasheria Tanganyika(TLS) Lawrence Masha ametengua uamuzi wake kwa kusema   kuwa  ameamua kuumuunga mkono mgombea mwenzake Tundu Lissu.

  Maamuzi hayo ameyafanya wakati alipokaribishwa ili kujinadi mbele ya wapiga kura wake  katika mkutano mkuu wa Tls  unaoendelea katika kituo cha mkutano cha kimataifa Aicc Jijini Arusha Leo.

  Aidha mwenyekiti wa uchaguzi amesema kuwa Kwa kuwa Lawrence Masha siyo mgombea tena haruhusiwi kuulizwa maswali tena.Uchaguzi utafanyika kesho siku ya jumamosi saa kumi na mbili asubuhi hadi saa tatu endelea kukaa karibu na sisi tutakuhabarisha kila kinachoendelea kutokea Arusha. 
  Pichani ni  Lawrance Masha Akiwa anamnadi Mgombea mweza Mh: Tundu lisu.Picha na Imma msumba
  Mgombea wa Urais wa Tls Mh: Victoria Mandari Pichani akiwa anajinadi na kuomba kura kwa wapiga kura wake.
  Pichani ni Mke wa Mh: Tundu Lisu Akiwa anachangia mada kwenye Mkutano wa Tls Arusha .
  Kutoka kulia ni Mh: Tundu lisu akiwa anateta jambo na wakili msomi Kibatala.
  Pichani ni wakili John Malya Akiwa anafuatilia kwa makini sera za mgombea wa urais wa Tls Tundu Lisu. 
  Baadhi ya wadau wa Sheria wakifuatilia kwa umakini mkutano wa Tls uliofanyika leo Jijini Arusha .Picha na Imma msumba

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: MASHA ATENGUA USHIRIKI WAKE TLS,AAMUA KUMUUNGA MKONO MGOMBEA MWENZAKE TUNDU LISSU Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top