728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Tuesday, March 14, 2017

  MAKONDA AFANYA ZIARA BONDE LA MTO MSIMBAZI,ATOA TAHADHARI

   Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa katika bonde la mto Msimbazi kukagua wakazi wa eneo hilo ambao wamepitiwa na hadha ya mafuriko yaliyotokana na mvua ilinyosha jana
   Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akikatiza kuvuka upande wa pili wa bonde mto msimbazi kujionea jinsi maji yalivyofanya uharibifu
   Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa na jopo la watumishi na wakazi wa jiji katika bonde la Mt Msimbazi
   Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam akivuka moja ya sehemu ambazo zina maji katika bonde la mto Msimbazi
   Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam akishuka kuelekea Bondeni kuangalia namna mvua zilizonyesha Dar es Salaam na kuleta madhara kwa wakazi hao
   Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akikatiza katika maeneo ya bonde la Mto Msimbazi
  Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam akizungumza na wajasilimali na wanawake wa bonde la mto Msimbazi ambao wanafanya biashara ya kuuza maembe.
   
  Na Ripota wa globu ya jamii

  Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewatahadharisha wakazi wa bonde la mto msimbazi kuwa kuwa mvua zinazo nyesha zitaweza kuendelea kuleta madhara kwa wakazi waishio mabondeni kutokana na uharibifu wa miundombinu ya maji.

  Makonda amesema hayo alipokuwa akizungumza na wakazi wa bonde la mto Msimbazi ambao walikusanyika kumsikiliza wakati alipokuwa akitembelea maeneo hayo.

  "la kwanza katika ngazi ya mkoa kulingana na utabiri wa hali ya mvua, zipo kati ya Milimita 30 hadi 35 na zikiendelea kuongezeka mpaka Milimita 50 maana yake hali itakuwa ni mbaya zaidi hivyo waswahili usema kinga ni bora kuliko tiba "Aamesema Makonda

  amesema kuwa wao kama Serikali chini ya Rais Magufuli wanategemea kupata fedha kutoka benki ya Dunia ili waweza kudhibiti na kutengeza mto msimbazi kupunguza Madhara.

  amesema hayo yanayo onekana leo ni tabia mbaya za kwetu wenyewe wanadamu kuwa wakaidi pindi tunavyoambiwa tusijenge mabondeni tunakuwa wabishi la pili tunaambiwa tuhakikishe kuwa atuharibu zile kingo za maji sisi tunaharibu na kuziba kisha kujenga

  ametaja kuwa maji hayo mengi hutokea katika maeneo mbalimbali ikiwemo mkoa wa pwani hasa katika eneo la kisarawe na kuhitaji kupita katika mto huu hivyo ukijengwa ndipo madhara haya  huonekana .
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: MAKONDA AFANYA ZIARA BONDE LA MTO MSIMBAZI,ATOA TAHADHARI Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top