728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Tuesday, March 21, 2017

  Kesi ya Wakurugenzi MSD kusikilizwa Aprili 18, mwaka huu.

  Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

  Kesi ya Matumizi mabaya ya ofisi inayomkabili Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MSD, Cosmas Aron Mwaifwani na Kaimu Meneja Manunuzi MSD, Frederick Rubanga Nicolaus itaanza kusikilizwa Aprili 18, mwaka huu.

  Hatua hiyo imefikiwa leo baada ya upande wa mashtaka kuwasomea washtakiwa hao maelezo ya awali.

  Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa, Aneth Mavika ameiambia mahakama kuwa, kesi leo imekuja kwa ajili ya washtakiwa kusomewa maelezo ya awali na wako tayari kuwasomea.

  Wakili Mavika amesoma melezo hayo mbale ya Hakimu Mkazi Mkuu Respicius Mwijage ambapo katika maelezo hayo, washtakiwa wamekubali maelezo yao binafsi na vyeo vyao na kasha kukana mashtaka yote yahayohusiana na kosa hilo la matumizi mabaya ya madaraka.

  Hivyo kesi hiyo namba 102 ya 2017 itaanza kusikilizwa kwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka Aprili 18, mwaka huu.7

  Awali ilidaiwa kuwa, kati ya Machi Mosi na 19, mwaka 2013 washtakiwa hao wakiwa Makao Makuu ya MSD yaliyopo Temeke kwa nafasi zao walitumia madaraka yao vibaya kwa kuandaa, kusaini mkatabata namba moja wenye kumbukumbu MSD/003/Q/G/2010/1011/60 wa Machi Mosi, 2013.

  Iliendelea kudaiwa kuwa, washtakiwa hao wanadaiwa kuandaa call of oder namba 2 yenye kumbukumbu MSD/003/Q/G/2010/2011/60 ya Machi 19, 2013 na kuisababishia kampuni ya H.H Hillal & Company Limited kupata manufaa ya milioni 482,266,000.

  Kesi hiyo itaendelea April 18, mwaka huu kwa shahidi wa kwanza wa upande wa jamuhuri kuanza kutoa ushahidi wake.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Kesi ya Wakurugenzi MSD kusikilizwa Aprili 18, mwaka huu. Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top